Historia ya Jibuti

Historia ya Jibuti inahusu eneo la Afrika Mashariki ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Jibuti.

Nchi ilikuwa koloni la Ufaransa kwa jina la Somalia ya Kifaransa, halafu (1967) Eneo la Kifaransa la Waafar na la Waisa, kutokana na majina ya makabila mawili makubwa zaidi ya eneo hilo.

Sababu ya kuanzishwa kwa koloni ilikuwa nia ya Ufaransa ya kuwa na bandari ya mji wa Jibuti karibu na Bab el Mandeb inayotawala mawasiliano kati ya Bahari Hindi na Bahari ya Shamu kuelekea Mfereji wa Suez.

Nchi ilipata uhuru tarehe 27 Juni 1977.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Jibuti kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.