Historia ya Lesotho
Historia ya Lesotho inahusu eneo la Kusini mwa Afrika ambalo wakazi wake leo wanaunda Ufalme wa Lesotho.
Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.
Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.
Lesotho ya sasa ilianza kupatikana mwaka 1822 chini ya chifu Moshoeshoe I aliyeungana na makabila mengine dhidi ya Shaka Zulu (1818-1828).
Baadaye nchi iliathiriwa na mahusiano na Waingereza na Makaburu wa . Koloni la Rasi (leo Afrika Kusini), yakiwemo mapigano ya mara kwa mara.
Wamisionari walioalikwa na Moshoeshoe I walianza kuandika na kuchapa kwa lugha ya Kisotho kati ya miaka 1837 na 1855.
Mwaka 1867 nchi ikawa chini ya malkia wa Uingereza kwa jina la Basutoland lakini mwaka 1869, Waingereza waliwaachia Makaburu nusu ya eneo la Basutoland.
Uhuru ulipatikana tena mwaka 1966, na nchi ikaitwa ufalme wa Lesotho.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Lesotho kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |