Hoorn ni mji wa mkoa Noord-Holland (Uholanzi wa Kaskazini) nchini Uholanzi. Mwaka 2014 kulikuwa na wakazi 71,699 walioishi kwenye eneo la km² 52 . Zaidi ya nusu ya eneo ni maji.

Mnara wa ulinzi kwenye bandari ya Hoorn

Hoorn iliundwa wakati wa karne ya 12 BK. Jina la mji humaanisha "pembe" linatokana na umbo la rasi ndogo inayoingia katika bahari na hapo mji ulianzishwa.

Shirika la Kiholanzi la Uhindi ya Mashariki lililoundwa kwa biashara ya viungo vya Asia lilikuwa na makao hapa Hoorn.

Mabaharia wengi na wavumbuzi muhimu walitoka mjini Hoorn. Kati yao alikuwa nahodha Willem Cornelisz Schouten aliyezunguka Amerika ya Kusini kwa jahazi na kuteua jina la Rasi Hoorn kwa heshima ya mji wake wa nyumbani.