Rasi Hoorn
Rasi Hoorn (kwa Kihispania Cabo de Hornos, kwa Kiingereza Cape Horn) ni rasi katika Chile kwenye sehemu ya kusini kabisa ya Amerika Kusini. Ni mahali ambako maji ya Pasifiki na maji ya Atlantiki hukutana.
Jina linatokana na mji wa Hoorn katika Uholanzi, kwa sababu walikuwa mabaharia kutoka mji ule waliochora rasi hii kwenye ramani mara ya kwanza na kuiteulia jina.
Rasi Hoorn ni ncha ya kusini ya funguvisiwa la Tierra de Fuegos (kwa Kiingereza fireland) ambavyo ni kundi la visiwa linalozunguka sehemu ya kusini ya Amerika Kusini bara.
Kabla ya kujengwa kwa Mfereji wa Panama njia ya rasi Hoorn ilikuwa njia muhimu kwa meli kati ya bahari mbili. Mizigo mingi iliyoelekea Kalifornia, Chile au Peru ilipita huko au kwenye mlangobahari wa Magellan uliopo takriban kilomita 120 upande wa kaskazini.
Rasi Hoorn ilitazamwa kuwa hatari kutokana na baridi, dhoruba kali, ukungu wa mara kwa mara, mkondo wa bahari na kutokea kwa siwa barafu kutoka Antaktiki. Zaidi ya meli na jahazi kubwa 800 ziliharibika huko kwa kuzama au kugonga miamba, na watu zaidi ya 10,000 walikufa katika ajali hizo. Ndiyo sababu ikaitwa "makaburi ya mabaharia".
Leo hii usafiri wa mizigo unapita katika mfereji wa Panama.
Viungo vya nje
hariri- Taarifa ya safari ya Jacob Le Maires mnamo 1621 pamoja na ramani na picha
- Ramani na wakazi asilia (National Library of Australia)
- Ramani ya bahari iliyotengenezwa na HMS Beagle, 1830–1834; National Maritime Museum, Greenwich Ilihifadhiwa 11 Agosti 2004 kwenye Wayback Machine.
- International Association of Cape Horners
- Chilean Brotherhood of Cape Horn Captains (Caphorniers)
- Adventurer George Kourounis' expedition to Cape Horn
- A monument at the end of the world Ilihifadhiwa 7 Februari 2012 kwenye Wayback Machine.—Chilean sculptor José Balcells' article (Spanish)
- Robert FitzRoy's commemorative plaque in Horn Island (image) Ilihifadhiwa 21 Oktoba 2010 kwenye Wayback Machine.
- Cape Horn, Tierra Del Fuego, Antarctica and South Georgia Ilihifadhiwa 19 Machi 2006 kwenye Wayback Machine.—antique charts of the Cape Horn region
- Sailing Way Down South – Ellen MacArthur's rendezvous at Cabo de Hornos
- Satellite image and infopoints Ilihifadhiwa 18 Septemba 2010 kwenye Wayback Machine. on BlooSee
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|