Hospitali ya Wasso
Hospitali ya Wasso ni hospitali inayopatikana Loliondo, wilaya ya Ngorongoro katika mkoa wa Arusha.
Ilianzishwa kama hospitali ya Umisheni na hayati Dr. Herbert Watschinger kutoka Austria. Huyu alikuwa ni Padri na Daktari ambaye lengo lake kubwa halikuwa kuhubiri bali lilikuwa ni kujikita katika kutoa misaada mbalimbali kwenye jamii ambazo hazikupata huduma muhimu za kijamii. Ndipo alipofanikiwa kuanzisha Hospitali hii mwaka 1964. Aliamua kuanzisha hospitali hii ikiwa ni kuleta usawa, ubora, urahisi kwa jamii. [1]
Marejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-12-04. Iliwekwa mnamo 2020-03-07.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |