Hoyce Temu

Balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa
(Elekezwa kutoka Hoyce Anderson Temu)

Hoyce Anderson Temu (alizaliwa katika Wilaya ya Ilala, jiji la Dar es Salaam, 20 Machi 1978[1]) alikuwa mshindi wa taji la urembo Tanzania mwaka 1999 na kuiwakilisha nchi ya Tanzania katika mashindano ya urembo wa dunia nchini Uingereza[2],anajulikana kama Mrembo wa Millenium wa mwaka 1999[3].

Pamoja na kuendeleza sanaa ya urembo nchini Tanzania, ni mtangazaji wa kipindi cha runingaː anaendesha Mimi na Tanzania[4] alichokianzisha mwaka 2011 kikiwa na lengo la kuyaibua matatizo ya watu wenye uhitaji ili waweze kupata msaada (fedha, faraja au fedha na faraja); mpaka tarehe 18 Machi 2016 kipindi hicho kimeweza kusaidia watu 1,000[5] na bado kinaendelea kusaidia watu zaidi.

Elimu na Uzoefu

hariri

Elimu yake ya sekondari amechukua katika shule ya Arusha na shule ya wasichana ya Zanaki[6].

Baada ya kumaliza elimu ya sekondari na kufaulu vizuri alipata udhamini [7] na kujiunga katika chuo cha Arizona State nchini Marekani kwa elimu ya juu na kuchukua shahada ya kwanza.

Baada ya kumaliza shahada ya kwanza alianza kufanya kazi kama meneja wa mambo ya ushirika[8]katika Benki ya Standard Charter na kuendelea kusoma chuo cha Diplomasia.

Baada ya kumaliza alijiunga katika chuo kikuu cha Mtakatifu Augustine na kuchukua elimu ya Mawasiliano ya Umma [9].

Alipomaliza, alichukua Shahada ya Uzamivu Johanesburg[10], nchini Afrika ya Kusini.

Pia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano cha Umoja wa Mataifa (UN), amehusishwa na kazi za kuisaidia jamii na mwaka 2014 siku ya wanawake Duniani taasisi ya MISA ilimtangaza[11] kama moja ya wanawake mashuhuri.

Viungo vya nje

hariri

Marejeo

hariri
  1. http://www.misstanzania.net/history.htm Ilihifadhiwa 29 Oktoba 2018 kwenye Wayback Machine.,
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-29. Iliwekwa mnamo 2018-10-20.
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-29. Iliwekwa mnamo 2018-10-20.
  4. http://www.mwananchi.co.tz/habari/Makala/Najivunia-miaka-tisa-ya-Mimi-na-Tanzania/1597592-4346684-format-xhtml-m4v6lc/index.html
  5. http://www.mwananchi.co.tz/habari/Makala/Najivunia-miaka-tisa-ya-Mimi-na-Tanzania/1597592-4346684-format-xhtml-m4v6lc/index.html
  6. http://www.thecitizen.co.tz/magazine/thebeat/Hoyce-temu-looks-at-her-reign-as-MIss-Tz/1843792-4148180-dbd21b/index.html
  7. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-26. Iliwekwa mnamo 2018-10-20.
  8. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-26. Iliwekwa mnamo 2018-10-20.
  9. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-26. Iliwekwa mnamo 2018-10-20.
  10. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-26. Iliwekwa mnamo 2018-10-20.
  11. http://www.tanzaniatoday.co.tz/news/hoyce-temu-among-top-misa039s-women-to-watch-2014rlm
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hoyce Temu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.