Huduma ya Ujasusi ya Kitaifa, Kenya
Huduma ya Ujasusi ya Kitaifa (kwa Kiingereza: National Intelligence Service, kifupi: NIS) ni shirika la upelelezi ndani na nje mwa Kenya ili kuhakikisha usalama wa nchi. Asili yake ilikuwa Tawi Maalum (kwa Kiingereza: Special Branch, kifupi: SB) iliyokuwa idara ya polisi kutoka mwaka 1952 hadi mwaka 1999 kama Idara ya Ujasusi.[1]
Historia
haririTawi Maalum (SB)
haririMwaka 1926, Idara ya Uchunguzi wa Jinai iliundwa na wakoloni na kuwa na tawi lenye jukumu la upelelezi. Kati ya Vita vikuu vya pili vya dunia hadi mwaka 1963, shughuli za SB zilijumuisha upelelezi wa wananchi waliokuwa wakidai uhuru, vuguvugu la vyama vya wafanyakazi na Mau Mau.
Serikali za nyakati za baada ya uhuru zilitumia SB kukandamiza wapinzani. Mwaka 1998, Huduma ya Ujasusi wa Usalama wa Kitaifa (kwa Kiingereza: National Security Intelligence Service, kifupi: NSIS) ilibuniwa na zaidi ya maafisa 170 kupigwa kalamu. Katika mwaka 1999, NSIS na Huduma ya Polisi zilitenganishwa, mamlaka ya NSIS ya kukamata washukiwa kuondolewa, na mahakama kuanzishwa ili isikize malalamiko dhidi ya SB.
Huduma ya Ujasusi ya Kitaifa
haririNIS iliundwa upya na Katiba ya Kenya ya Mwaka 2010. Inaongozwa na Sheria ya Huduma ya Ujasusi ya Kitaifa ya mwaka 2012.
Majukumu
haririAngalia pia
haririMarejeo
hariri- ↑ "NSIS Historical Background". National Security Intelligence Service. 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Desemba 2007.
{{cite web}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help)