Hugo Lloris

Mchezaji mpira wa Ufaransa

Hugo Hadrien Dominique Lloris (alizaliwa 26 Desemba 1986 [1]) ni mchezaji wa soka wa Ufaransa ambaye anacheza kama golikipa wa klabu ya Tottenham Hotspaurs na timu ya taifa ya Ufaransa [2], Ndiye nahodha mkuu wa pande zote mbili anazochezea.

Hugo Lloris.

Lloris alianza kazi yake ya mpira wa miguu alipokuwa na umri wa miaka sita na katika klabu ya Nice ya Ufaransa. 29 Mei, 2008 alihamia Lyon kwa milioni 8.5 kwa mkataba wa miaka mitano.

Lloris akiudaka mpira uliopigwa na Oscar wa chelsea.

Lloris alianza kuchezea klabu yake mnamo 10 Agosti 2008 dhidi ya Toulouse. Alimaliza msimu kwa kufungwa mabao 27 tu kwenye ligi na kutofungwa mechi 16 kati ya 37.

Lloris alisaini mkataba na Tottenham Hotspurs mnamo 31 Agosti 2012 kwa € milioni 15 kwa miaka miwili, Kifikia 2014 aliongeza mkataba wa miaka mitano mpaka Julai 2019 na meneja Mauricio Pochettino akampa unahodha wa moja kwa moja mpaka kuondoka kwake. Mwezi julai 2019 bosi wa Tottenham alionekana kufurahishwa na huduma ya Lloris na kumuongezea mshahara na kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu hadi 2022.

Marejeo

hariri
  1. "Squad List: FIFA World Cup Qatar 2022: France (FRA)" (PDF). FIFA. 15 Novemba 2022. uk. 12. Iliwekwa mnamo 15 Novemba 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Hugo Lloris named as France's Euro 2012 captain", Sporting News, 28 February 2012. Retrieved on 2022-12-07. Archived from the original on 2012-07-11. 
  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hugo Lloris kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.