Machozi ni jina la albamu ya kwanza ya mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania, Lady Jay Dee. Albamu imetoka mwaka wa 2000. Albamu imetayarishwa katika studio za Master Jay, jijini Dar es Salaam. Hii ni albamu ya kwanza ya muziki wa kizazi kipya kwa kutumia gharama kubwa sana katika utayarishaji kuliko albamu zote zilizotoka mwanzoni mwa miaka ya 2000. Wakati ndio hasa Smooth Vibe Project ilikuwa inasimamia kazi za wasanii wengi wa Tanzania.[1]

Machozi
Machozi Cover
Studio album ya Lady Jay Dee
Imetolewa 2000
Imerekodiwa 2000
Aina Bongo Flava, R&B
Lebo MJ Records
Mtayarishaji Master Jay
Wendo wa albamu za Lady Jay Dee
"Machozi"
(2000)
"Binti"
(2003)

Orodha ya nyimbo hariri

  • Machozi (remix)
  • Nalia
  • Penzi la milele
  • Pumziko
  • Waweza kwenda (Rajabu's mix)
  • Nakupenda
  • Nimekubali (akiwa na Ray C)
  • Matatizo
  • Tatiza
  • Shida
  • Umuhimu wako
  • Waweza kwenda (JM mix)

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. Machozi katika wavuti ya Mzibo.net