Kipanya-milia

(Elekezwa kutoka Hybomys)
Kipanya-milia
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wanyama wagugunaji)
Nusuoda: Myomorpha (Wanyama kama panya)
Familia: Muridae (Wanyama walio na mnasaba na panya)
Nusufamilia: Murinae (Wanyama wanaofanan na vipanya-miiba)
Jenasi: Hybomys
Thomas, 1910
Ngazi za chini

Spishi 6:

Vipanya-milia ni wanyama wagugunaji wa jenasi Hybomys katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae ambao wanatokea katika misitu ya mvua ya Afrika ya Magharibi na ya Kati.

Maelezo

hariri

Manyoya ya mgongo huwa aina ya kahawia kwa kawaida, tumbo ni jeupe au njano. Urefu wa mwili ni mm 100-160 mm, urefu wa mkia mm 85-130 na uzito g 40-80.

Vipanya-milia hukiakia wakati wa mchana na usiku. Wanaishi ardhini, haswa katika maeneo yenye majani mengi na takataka kama haya ardhini. Pengine hulala katika miti iliyooza. Wanyama hao hula matunda hasa.

Spishi

hariri