Kipanya-miiba

Jenasi ya vipanya katika familia Muridae.
Kipanya-miiba
Kipanya-miiba wa Rasi (Acomys subspinosus)
Kipanya-miiba wa Rasi (Acomys subspinosus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wanyama wagugunaji)
Nusuoda: Myomorpha (Wanyama kama panya)
Familia: Muridae (Wanyama walio na mnasaba na panya)
Nusufamilia: Deomyinae (Wanyama wanaofanan na vipanya-miiba)
Jenasi: Acomys
I.Geoffroy, 1838
Ngazi za chini

Spishi 21:

Vipanya-miiba ni wanyama wagugunaji wa jenasi Acomys katika nusufamilia Deomyinae ya familia Muridae walio na manyoya magumu kama miiba. Wanatokea katika Afrika na Mashariki ya Kati kwenye majangwa na maeneo mengine makavu, pengine misitu mikavu na mara nyingi maeneo yenye mawe na miamba.

Maelezo

hariri

Vipanya-miiba hufanana sana na vipanya wa kawaida wa jenasi Mus, lakini hutofautiana kwa kuwa na manyoya magumu sana, kama miiba, na mkia mfupi zaidi ambao wanaweza kumwaga ili kuchopoka. Wana urefu wa sm 8-17.5 na mkia wa sm 4-12 na uzani wa g 18-90, yote kulingana na spishi. Kwa kawaida manyoya huwa kahawia au kijivu au yenye rangi ya nyekundu/machungwa kidogo, mara chache nyeupe au nyeusi; upande wa chini ni mweupe. Huwa na masikio makubwa na pua iliyoelekezwa zaidi kuliko vipanya wa kawaida.

Chakula

hariri

Vipanya hao hula mbegu, maua, mimea ya jangwani, konokono, wadudu na mizoga, lakini spishi kadhaa hula wadudu hasa. Kwa kawaida hawakunywi na hupata maji kutoka kwa chakula chao. Wanatoa mkojo uliokolea ili kuzuia upoteaji wa maji.

Makazi

hariri

Makazi ya vipanya-miiba ni maeneo makavu, kama majangwa, savana na vichaka na misitu mikavu, mara nyingi yenye miamba. Hukiakia usiku au alasiri na alfajiri sana. Spishi kadhaa zinaweza kukiakia mchana. Kwa asilia huishi miaka mitatu kwa wastani, lakini kifungoni wanaweza kuishi zaida ya miaka mitano.

Kipindi cha ujauzito ni wiki 3-5. Majike huzaa wachanga 2-5 ambao wana manyoya mafupi tayari na macho yaliyofunguka. Majike wanaweza kupandana tena mara tu baada ya kuzaa.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za Asia

hariri
  • Acomys cilicicus
  • Acomys dimidiatus
  • Acomys minous
  • Acomys nesiotes
  • Acomys russatus