Kipanya-misitu
(Elekezwa kutoka Hylomyscus)
Kipanya-misitu | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 21:
|
Vipanya-misitu ni wanyama wagugunaji wa jenasi Hylomyscus katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae ambao wanatokea katika misitu na maeneo yenye midambi ya Afrika kusini kwa Sahara.
Maelezo
haririVipanya hawa wana masikio makubwa yenye mviringo na mkia mrefu na mwembamba. Urefu wa mwili ni mm 55-120, urefu wa mkia ni mm 75-175 na uzito ni g 6-42. Manyoya yao ni laini na kahawia hadi kahawianyekundu mgongoni na kijivu iliofifia tumboni.
Hukiakia usiku na wanaishi kwenye miti. Hula matunda, mbegu na wadudu.
Spishi
hariri- Hylomyscus aeta, Kipanya-milia wa Uganda (Beaded wood mouse) – Burundi, Uganda
- Hylomyscus alleni (Allen's wood mouse)
- Hylomyscus anselli, Kipanya-misitu wa Ansell (Ansell's wood mouse) – Tanzania
- Hylomyscus arcimontensis, Kipanya-misitu wa Tao la Mashariki (Arc Mountain wood mouse) – Tanzania
- Hylomyscus baeri (Baer's wood mouse)
- Hylomyscus carillus (Angolan wood mouse)
- Hylomyscus denniae, Kipanya-misitu wa Ruwenzori (Montane wood mouse) – Uganda
- Hylomyscus endorobae, Kipanya-misitu Miguu-midogo (Small-footed wood mouse) – Kenya
- Hylomyscus grandis (Mount Oku wood mouse)
- Hylomyscus heinrichorum (Heinrich's wood mouse)
- Hylomyscus kerbispeterhansi, Kipanya-misitu wa Ml. Elgon (Kerbis Peterhans's wood mouse) – Kenya, Uganda
- Hylomyscus mpungamachagorum, Kipanya-misitu wa Mahale (Mahale wood mouse)
- Hylomyscus pamfi (Pamfi wood mouse)
- Hylomyscus parvus (Little wood mouse)
- Hylomyscus pygmaeus (Pygmy wood mouse)
- Hylomyscus simus (Flat-nosed wood mouse)
- Hylomyscus stanleyi, Kipanya-misitu wa Stanley (Stanley's wood mouse)
- Hylomyscus stella, Kipanya-misitu wa Stella (Stella wood mouse) – Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda
- Hylomyscus thornesmithae (Mother Ellen's wood mouse)
- Hylomyscus vulcanorum, Kipanya-misitu wa Volkano (Volcano wood mouse) – Burundi, Rwanda, Uganda
- Hylomyscus walterverheyeni (Walter Verheyen's mouse)