"I Have a Dream" ni wimbo kutoka kwa kundi kutoka nchini Swedish linaoimba muziki wa aina ya pop linaloitwa ABBA. Wimbo huu ulitungwa ba Benny Andersson & Bjorn Ulvaeus na uliimbwa na kundi hilo katika albamu yao ya mwaka 1979 iliyoitwa Voulez-Vous. [Huku [Anni-Frid Lyngstad]] akiimba viitikio vya wimbo huo. Wimbo huo ulitoka kama single mwezi desember mwaka 1979, ikijumuishwa na toleo la moja kwa moja kutoka kwa "Take a Chance on Me" as the B-side).

“I Have a Dream”
“I Have a Dream” cover
Single ya ABBA
B-side "Take a Chance on Me" (Live)
Muundo Single
Aina Pop ballad
Urefu 4:45
Mtunzi Benny Andersson
Björn Ulvaeus
Certification Gold (UK), Gold (Netherlands)

Wimbo wa "I Have A Dream" ulikuwa ni single ya mwisho kutoka kwa kundi la BBA katika mwaka"1970. Muongo ambao kundi hili lilipata mafanikio kuliko kundi lingine duniani. Wimbo wa "I Have a Dream" sio tu wimbo pekee wa kundi hili unaojumuisha sauti za wanamuziki wote ndani ya kundi hilo, lakini pia hujumuisha pia sauti za kwaya ya watoto. Wimbo wa "I Have a Dream pia umejumuishwa katika albamu ya kundi la BBA inayoitwa ABBA Gold: Greatest Hits lakini pia katika muziki wa Mama Mia.

Kutolewa kwa Single

hariri

Kumekuwa na hisia kuwa wimbo wa "I Have a Dream" asili yake haukutengenezwa kama single, tayari kulikwa na nyimbo tatu kutoka katika albamu ya Voulez-Vous. Albamu nyingine kuwahi kuwa na single zipatazo nne ni pamoja na ile ya ABBA ya mwaka 1975, iliyokuwa ikijumisha pande mbili, wimbo wa "I Have a Dream" ulikuwa ni wimbo wa saba katika albamu iliyokuwa na nyimbo kumi iliyoitwa Voulez-Vous amabyo ilitoka kama single nchini Uingereza.

Pia wimbo huo haukujumuishwa katika albamu yao ya Greatest Hits Vol.2 ambayo ilitoka wiki mbili tu kabla. Kwa hali hiyo, wimbo huu unadhaniwa kuwa ulikuwa ni wimbo wa ziada tu, katika kufidia nyimbo za Christmas na katika ziara yao ya mwaka 1979. Halikadhalika kundi la BBA halikufanya video ya wimbo huo, japokuwa walifanya katika ule ulioimbwa katika lugha ya kihispania yaani "Estoy Soñando". Ilikuwa si kawaida kwa kundi la BBA kuacha kutengeneza video ya nyimbo iliyotolewa rasmi. Toleo la Kihispania lilitolewa katika video katika studio za Polar Music Studios katika siku hiyo hiyo kama ilibyokuwa kwa video ya wimbo wa "Gimme! Gimme! Gimme!" ambao pia uliwaonesha vijana wa BBA wakiwa katika nguo hizo hizo

Kama wimbo wa "I Have a Dream" Ulitengenezwa kama single, ni wazi kuwa ungetengenezewa video yake katika kipindi kile kile.

Matoleo

hariri

Onesha la moja kwa moja la wimbo wa "Take a Chance on Me" kwa upande wa pili ulikuwa ni moja wa ya nyimbo tatu zilizopangwa kurekodiwa.Kutokana na kutoka muda mfupi tu baada ya onesho, wimbo huu unaaminika kuwa ulirekodiwa katika hali ya uhalisia. Kijisehemu kidogo katika upande wa pili, kinachohusisha sauti za mazungumzo kutoka kwa kundi hili, kilijumuishwa katika toleo la Australia. Toleo la pili la limeweza kutolewa katika kiwango cha kimataifa na pia umetolewa kama nyongeza katika albamu ya The Albam. Hatimaye katika hatua ya tatu, wimbo huu ulijuishwa katika ABBA Live iliyotoka mwaka 1986.

Mapokezi

hariri

Wimbo wa "I Have a Dream" uliweza kuvuma duniani kote, na kuweza kufika katika nafasi ya kwanza katika chati za nchini, Austria, Ubelgiji, Netherlands, na Switzerland wakati ikishika nafasi ya pili katika chati ya muziki ya nchini Uingereza, ambapo uilishindwa kufikia nafasi ya kwanza kutokana na single ya kundi la Pink Floydna wimbo wa "Another Brick in the Wall (Part 2)". Wimbo wa "I Have a Dream" ulifanikiwa kufika hadi nafasi ya saba nchini Ireland, Rhodesia, Afrika ya Kusini na Ujerumani ya Magharibi, huku ikiwa katika nafasi ya kwanza katika chati ya muziki ya Adult Contemporary chart in Canada. Toleo katika ligha ya Kihispania "Estoy Soñando", ilifanikiwa kufika nafasi ya kumi na tano nchini Uhispania na pia uliweza kufika katika nyimbo tano bora katika nchi za Argentinana Mexico.

Wimbo wa "I Have a Dream" haukutolewa kama toleo la kibiashara nchini Marekanilakini uliweza kupendwa zaidi katika radi mbalimbali kama vile Easy Listening & Adult Contemporary. Mwimbaji wa nyimbo za dini Cristy Lane aliurudia wimbo huo na kufanikiwa kufaka katika nafasi ya 17 nchini Marekani katika chati ya country singles chart mwaka 1981.

Chati (1979/1980) Nafasi
Australian Singles Chart 64
Austrian Singles Chart 1
Belgian Singles Chart 1
British Singles Chart 2
Canadian Adult Contemporary Chart 1
Cypriot Singles Chart 1
Dutch Singles Chart 1
Eurochart Hot 100 Singles 1
French Singles Chart 42
German Singles Chart 4
Irish Singles Chart 2
Rhodesian Singles Chart 7
South African Singles Chart 3
Swiss Singles Chart 1

Walioimba baadae

hariri

Waimbaji mbalimbali wameimba wimbo huu kama vile.

  • Ulirekodiwa na dansband Streaplers, huku mashairi yakiandikwa katika lugha ya Sweden na Ingela Forsman, "Jag har en dröm", Ulishika nafasi ya kwanza nchini Sweden katika chati ya Svensktoppen kwa kipindi cha wiki 17 kuanzia 31 Mei - 6 Desemba 1987

Toleo la Westlifen

hariri
“I Have a Dream"/"Seasons in the Sun
 
Single ya Westlife
Muundo CD single
Aina Pop ballad, teen pop
Mtunzi Benny Andersson / Björn Ulvaeus
Certification Platinum (UK)
Mwenendo wa single za Westlife
"Flying Without Wings"
(1999)
(3)
"I Have a Dream / Seasons in the Sun"
(1999)
(4)

Westlife walitoa wimbo huu kwa mara ya pili mwezi december mwaka 1999, ikiwa ni miaka ishirini tangu wimbo huu uimbwe na kundi la ABBA. wimbo huu ukawa wimbo wa nne wa kundi la Westlife kuwahi kufika nafasi ya kwanza katika chati ya muziki ya Nchini Uingereza, halikadhalika wimbo huu ulifanikiwa kuwa wimbo wa kwanza katika nyimbo za Christmas kwa mwaka 1999 na kuweza kushika nafasi hiyo hadi mwezi wa kwanza mwaka 2000. Hadi sasa wimbo huu umeshika nafasi ya 47, katika nyimbo za Christmas zilizowahi kufika nafasi ya kwanza. Pia wimbo huu ulikuwa wimbo wa mwisho katika kuachia nafasi ya kwanza kwa mwaka 1990

Wimbo huu pia, unashika nafasi ya 26, katika nyimbo zinazoongoza kwa mauzo nchini Uingereza Mwaka 2001, kama sehemu ya msaada katika kufanya harambee ya shirika la UNICEF wimbo huu ulirekodiwa kwa mara ya pili na kuingiza sauti ya mwanamuziki wa mtoto wa nchini Indonesia, Sinna Sherina Munaf. Wimbo huu umefanikiwa kuuza zaidi ya nakala 600,000 nchini Uingereza.

Mtiririko wa nyimbo

hariri
  1. "I Have a Dream" (Single Remix) - 4:06
  2. "Seasons in the Sun" (Single Remix) - 4:10
  3. "On the Wings of Love" - 3:22

Mtiririko wa matamasha

hariri
Nchi/Nafasi Ulipata
Nafasi
German Singles Chart 24
Irish Singles Chart 1
New Zealand Singles Chart 10
Swedish Singles Chart 15
Swiss Singles Chart 18
UK Singles Chart 1
UK Radio Airplay Chart 7

Viunga vya njes

hariri

Marejeo

hariri