Igosi ni kata ya Wilaya ya Wanging'ombe katika Mkoa wa Njombe, Tanzania. Msimbo wa posta ni 59310.

Kata ya Igosi
Nchi Tanzania
Mkoa Njombe
Wilaya Wanging'ombe
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 7,574

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 7,574 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,204 [2] walioishi humo.

Igosi ina vitongoji sita: Mlimani, Ng'ange, Mkangacha, Igelango, Ndulamo, Majengo.

Wakazi wanasema jina Igosi lina maana ya Vagosi, yaani wanaume kwa lugha yao. Hii ni kwa sababu wakati uliopita kulikuwa na mashindano ya kutafuta wababe. Watu wa vijiji jirani walikuwa wakifika kijijini kujipima lakini walikuwa wakishindwa na kukiri, "Pene pala pali vagosi".

Marejeo

hariri
  1. https://www.nbs.go.tz, uk 212
  2. "Sensa ya 2012, Njombe - Wanging'ombe DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-28.
  Kata za Wilaya ya Wanging'ombe - Tanzania  

Igima | Igosi | Igwachanya | Ilembula | Imalinyi | Itulahumba | Kidugala | Kijombe | Kipengele | Luduga | Makoga | Malangali | Mdandu | Saja | Udonja | Uhambule | Uhenga | Ulembwe | Usuka | Wangama | Wanging'ombe


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Igosi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.