Ilembula ni kata ya Wilaya ya Wanging'ombe katika Mkoa wa Njombe, Tanzania. Msimbo wa posta ni 59305.

Kata ya Ilembula
Nchi Tanzania
Mkoa Njombe
Wilaya Wanging'ombe
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 18,174

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 15,642 [1] walioishi humo.

Wenyeji walio wengi ni Wabena wanaolima hasa mahindi na maharagwe. Vinywaji vinavyopendwa ni ulanzi, pombe na togwa.

Ndani ya kata kuna vijiji vya Ilembula Kati, Iponda, Igelehedza na Igula. Ilembula Kati, Igelehedza na Igula kuna shule ya msingi. Taasisi kubwa ni hospitali ya Kilutheri pamoja na chuo chake.

Dini Edit

Ilembula imekuwa kitovu cha kazi ya Walutheri katika Ubena tangu mwaka 1906, wamisionari Wajerumani walipofika. Leo hii Ilembula Kati ni makao makuu ya Jimbo la Kilutheri ndani ya Dayosisi ya Kusini KKKT. Kanisa hili linaendesha hospitali yenye vitanda 240 pamoja na chuo cha wauguzi chenye wanafunzi 143.[2]

Kanisa Katoliki lina kitovu chake kwenye kijiji cha Igelehedza pamoja na shule ya chekechea na shule ya maarifa ya nyumbani.

Madhehebu mengine, kama vile Wapentekoste, Wasabato na Mashahidi wa Yehova, wako pia hata kama si wengi.

Nao Waislamu wako: wana msikiti katika Igelehedza.

Marejeo Edit

  1. Sensa ya 2012, Njombe - Wanging'ombe DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-28.
  2. www.ilembulanursing.ac.tz

Viungo vya nje Edit

  Kata za Wilaya ya Wanging'ombe - Tanzania  

Igima | Igosi | Igwachanya | Ilembula | Imalinyi | Kidugala | Kijombe | Kipengele | Luduga | Makoga | Mdandu | Saja | Uhambule | Ulembwe | Usuka | Wangama | Wanging'ombe


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ilembula kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.