Kidugala
Kidugala ni kata ya Wilaya ya Wanging'ombe katika Mkoa wa Njombe, Tanzania. Msimbo wa posta ni 59312.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 5,580 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 4,838 [2] walioishi humo.
Wakazi wa Kidugala ni Wabena.
Mwanzo wa misioni ya Kilutheri
haririKatika karne ya 19 kulikuwa na makao makuu ya Mwene Ngele (au Ngera). Huyu alikaribisha wamisionari wa Shirika la Misioni ya Kilutheri ya Berlin walioanzisha kituo chao kwenye mwaka 1898. Kutoka hapo Kidugala iliendelea kuwa kitovu cha misioni ya Kilutheri katika Ubena.
Mwaka 1904 wamisionari walianzisha shule kwa ajili ya wainjilisti iliyoendelea kuwa Chuo cha Biblia baadaye. Kanisa lilijengwa mwaka 1908, karahana ya kuchapa vitabu mwaka 1910. Mwaka 1911 hospitali ya misioni ilikamilika. Kufikia mwaka 1914 ushirika wa Kilutheri ulikuwa na Wakristo 114 na wakatekumeni 71.[3]
Tanbihi
hariri- ↑ https://www.nbs.go.tz, uk 212
- ↑ "Sensa ya 2012, Njombe - Wanging'ombe DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-28.
- ↑ Altena, uk. 180
Marejeo
hariri- Thorsten Altena: "Ein Häuflein Christen mitten in der Heidenwelt des dunklen Erdteils". Zum Selbst- und Fremdverständnis protestantischer Missionare im kolonialen Afrika 1884-1918 (= Internationale Hochschulschriften; Bd. 395), Münster: Waxmann 2003, 531 S., 12 Abb., 1 CD-Rom, ISBN 3-8309-1199-8
Kata za Wilaya ya Wanging'ombe - Tanzania | ||
---|---|---|
Igima | Igosi | Igwachanya | Ilembula | Imalinyi | Itulahumba | Kidugala | Kijombe | Kipengele | Luduga | Makoga | Malangali | Mdandu | Saja | Udonja | Uhambule | Uhenga | Ulembwe | Usuka | Wangama | Wanging'ombe |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kidugala kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |