Injili ya Yakobo ni kitabu[1] cha dini ya Ukristo kilichoandikwa kwa Kigiriki miaka 140-170 hivi BK (labda 145).

Pengine kinaitwa majina mengine, mojawapo "Kuzaliwa kwa Maria"[2]. Hii ni kwa sababu kinasimulia hasa uzazi (sura 1-8) na utoto wa Bikira Maria (sura 9-16), mbali ya utoto na uzazi wa Yesu (sura 17-24).

Ni cha kwanza kusema juu ya ubikira wake wakati wa kumzaa Yesu na baada ya hapo[3].

Ingawa mwandishi anajidai kuwa Yakobo Mdogo[4], wataalamu wanapinga neno hilo. Ingawa kitabu kilienea sana na kubaki hadi leo katika nakala nyingi za tafsiri mbalimbali, hakikukubaliwa kama sehemu ya Biblia ya Kikristo[5]. Sababu kuu inaweza kuwa ile ya kuchelewa kutungwa, baada ya wakati wa Mitume wa Yesu kwisha.

Baadhi ya masimulizi ya kitabu hicho yameingia katika Kurani na katika desturi za Kikristo, kama vile Pango la Noeli wakati wa Kuzaliwa kwa Yesu ambalo kwa kawaida linaonyesha uwepo wa ng'ombe na punda kama inavyosimuliwa na Injili ya Yakobo (18)[6].

Tanbihi hariri

  1. Porter, J. R. (2010). The Lost Bible. New York: Metro Books. uk. 134. ISBN 978-1-4351-4169-8. 
  2. Bart D. Ehrman, " Lost Scriptures: Books that did not make it into the New Testament" p.63
  3. Luigi Gambero, "Mary and the fathers of the church: the Blessed Virgin Mary in patristic thought" pp.35-41
  4. http://www.gnosis.org/library/gosjames.htm
  5. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-26. Iliwekwa mnamo 2016-09-08. 
  6. Wilhelm Schneemelcher, Robert McLachlan Wilson, New Testament Apocrypha: Gospels and related writings, Westminster John Knox Press, 2003, ISBN 0-664-22721-X, p. 65.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Injili ya Yakobo kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.