Pango la Noeli
Pango la Noeli (au pango) ni sanaa inayoonyesha jinsi Yesu Kristo alivyozaliwa.
Hiyo ni kadiri ya desturi za Karne za Kati, ambazo asili yake ni Fransisko wa Asizi (1182-1226).
Ndiye aliyeandaa pango hai akitumia watu na wanyama hai ili yeye na watu wa Greccio wajisikie zaidi washiriki wa tukio la usiku wa Noeli (1223).
Kabla yake picha na sanamu za uzazi wa Yesu zilikuwa zinahusu zaidi maadhimisho ya liturujia kuliko uhalisia wa tukio la Bethlehemu.
Kumbe Fransisko, aliyewahi kuhiji katika Nchi takatifu ya Israeli, alipenda hata wasiofika huko waelewe zaidi hali ilivyokuwa.
Uanzishaji wenyewe
haririBaada ya kanuni aliyoliandikia shirika lake kuthibitishwa na Papa Honori III tarehe 29 Novemba 1223, Fransisko alikwenda Greccio kujitafutia kimya na upweke. Ndipo alipopata wazo la kuadhimisha Noeli kwa namna mpya ili kuitia maanani zaidi.
Kwa msaada wa mtawala wa kijiji hicho, kwa ushirikiano wa wananchi na kwa mahudhurio ya ndugu wengi, liliandaliwa pango lenye majani makavu, ng’ombe na punda, halafu ikaadhimishwa Misa ambapo Fransisko, akiwa shemasi, alisoma Injili na kuhubiri kwa utamu mkubwa.
Lengo lilikuwa kuwafanya Wakatoliki wote wakumbuke jinsi Mwana wa Mungu alivyojishusha duniani, si tu kwa kujifanya mtu, bali pia kwa namna alivyozaliwa na alivyoishi. Chaguo lake la ufukara lilitegemea ukweli wa maisha ya Yesu kama mtu wa mwisho na mtu wa mateso.
Baada ya miezi michache ufuasi wake huo wa moja kwa moja ukaja kuthibitishwa na madonda matano aliyotiwa kiajabu juu ya mlima La Verna.
Mapango yasiyo hai
haririBaada ya hapo mapango yalianza kutengenezwa kwa sanamu (labda Arnolfo wa Cambio alitangulia kufanya hivyo kati ya 1290 na 1292.
Marejeo
hariri- Gerhard Bogner: Das neue Krippenlexikon. Wissen - Symbolik - Glaube. Ein Handbuch für den Krippenfreund. Fink, Lindenberg 2003 ISBN 3-89870-053-4
- Erich Egg, Herlinde Menardi: Das Tiroler Krippenbuch. Die Krippe von den Anfängen bis zur Gegenwart. 2. Aufl. Tyrolia, Innsbruck 2004 ISBN 3-7022-2604-4
- Ursula Pfistermeister: Barockkrippen in Bayern. Theiss, Stuttgart 1984 ISBN 3-8062-0398-9
- Alfons Rudolph, Josef Anselm Adelmann von Adelmannsfelden: Schwäbische Barockkrippen. Theiss, Stuttgart 1989 ISBN 3-8062-0815-8
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Pango la Noeli kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |