Kuzaliwa kwa Bikira Maria

Kuzaliwa kwa Bikira Maria ni sikukuu inayoadhimishwa tarehe 8 Septemba katika Kanisa Katoliki[1] na vilevile katika makanisa ya Waorthodoksi, ambako inaorodheshwa kati ya sherehe kuu.

Picha takatifu ya kuzaliwa kwa Mama wa Mungu.

Tukio hilo halisimuliwi na Biblia ya Kikristo, ila na Injili ya Yakobo, sura 1-5.

Kwa vyovyote, mama wa Yesu alizaliwa kweli kutoka uzao wa Abrahamu na taifa la Israeli katika karne ya 1 KK.

Tukio hilo liliandaa kabisa kuzaliwa kwa Yesu Kristo kwa kuwa Bikira Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ndiye anayesadikiwa kuwa mzazi wa Mwana wa Mungu aliyejifanya mtu ili kukomboa binadamu wote kutoka utumwa wa dhambi uliowapata tangu mwanzo kabisa[2].

Tanbihi

hariri
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kuzaliwa kwa Bikira Maria kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.