Ipelele ni kata ya Wilaya ya Makete katika Mkoa wa Njombe, Tanzania. Ni eneo dogo sana lenye vijiji sita yaani Ubiluko, Ipelele, Makwaranga, Mbanga, Makeve na Missiwa. Msimbo wa posta ni 59520.

Kata ya Ipelele
Nchi Tanzania
Mkoa Njombe
Wilaya Makete
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 4,890

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 4,890 [1] walioishi humo. Kata hiyo ina kabila dogo liitwalo Wamagoma.

Wenyeji wa eneo hilo wanajishughulisha na kilimo cha mahindi, ngano, njegere na viazi. Hata hivyo inasemekana kuwa walikuwa wafugaji wa ng'ombe wakubwa katika milima ya Ikata na Magoma; mpaka sasa ufugaji upo ila si sawa na zamani.

Marejeo hariri

  1. Sensa ya 2012, Njombe - Makete DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2021-01-16.
  Kata za Wilaya ya Makete - Tanzania  

Bulongwa | Ikuwo | Iniho | Ipelele | Ipepo | Isapulano | Itundu | Iwawa | Kigala | Kigulu | Kinyika | Kipagalo | Kitulo | Lupalilo | Lupila | Luwumbu | Mang'oto | Matamba | Mbalatse | Mfumbi | Mlondwe | Tandala | Ukwama


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ipelele kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.