Irini Merkouri (Kwa Kigiriki: Ειρήνη Μερκούρη, inatamkwa [iˈrini merˈkuri]; amezaliwa Ilion, Athens, 28 Mei 1981) ni mwimbaji wa pop na laika toka Ugiriki mwenye asili ya Wahindi wa Ulaya.[1]

Maisha ya awali

hariri

Merkouri alianza kuonyesha kupendelea kuwa mwimbaji katika umri mdogo sana na katika umri wa miaka saba angeweza kuwaiga waimbaji wote ambao angewaona kwenye televisheni.[2]

2001 - 2003: Albamu ya kwanza na Meine Mazi Mou Apopse

hariri

Irini Merkouri alisaini mkataba na Sony Music Greece na kurekodi albamu yake pekee Na Fysai I Anixi mnamo Novemba 2001. Kama sehemu ya hii albamu aliimba wimbo wa pamoja "Dio Mas" na Antonis Remos na toleo la Kigiriki kwa wimbo wa Kifaransa "Si Tu Ouvres Tes Bras" ujulikanao kama "Iparhi Kai Theos". Albamu ilijumuisha jumla ya nyimbo kumi na mbili ikijumuisha nyimbo kali "Syntelia" na "Foties Anapste". Mnamo Juni 2003, Merkouri aliachia albamu yake ya pili ya studio, ijulikanayo kama Mine "Mazi Mou Apopse" (Kaa Pamoja Nami Usiku Huu). Ilijumuisha nyimbo 12 na ilijuisha marudio ya "Syntelia" ambao uliongoza kupata muda wa kuchezwa hewani kwenye chati kwa miezi 3 mfululizo. Albamu pia ilijumuisha nyimbo kali "Ematha Na Zo Horis Esena" na "Meine Mazi Mou Apopse".

2004: Sarbel na Palirroia

hariri

Mnamo 2004, Merkouri alishirikishwa katika "Se Pira Sovara" ya Sarbel. Kwenye wimbo wa CD ileile Merkouri na Sarbel waliachia wimbo wa pili wa pamoja ujulikanao kama "Agapi Mou Esi". Mnamo Juni 2004, Merkouri aliachia albamu yake ya tatu ya studio iliyoitwa Palirroia, ambayo ilijumuisha nyimbo 15 mpya. Wimbo wa kwanza kupiga mawimbi ya hewa ulikuwa "Ela", nyimbo yenye mchanganyiko wa laika ya kisasa na chembechembe za ragga Wimbo wa pili , "Pou Na Fantasto" ulikuwa kipande cha kwanza cha video ya albamu na ulikuwa mkali katika vilabu vyote Ugiriki. Wimbo wa tatu, "Krata Me Ksana", uliandikwa na Takis Damashis na kwa msaada wake Merkouri ulipata tuzo ya "Best Pop Singer" (Mwimbaji Bora wa Pop).

2005 - 2009: Aneta, Argies, na “Nai”

hariri

Mnamo Julai 7, 2005, Merkouri aliachia albamu yake ya studio, iliyoitwa "Aneta" (Kwa raha). Ilikuwa na nyimbo kutoka kwenye albamu zake zilizopita na pia nyimbo mpya.http:[3] Mwaka 2006 ulileta albamu ya studio ya nne ya Merkouri, iliyoitwa Argises (Ulichelewa). Ilikuwa na nyimbo 13 mpya ikijumuisha nyimbo kama "Pame Gi'Alla" na "Miso Lepto" ambazo zikawa kipande cha video. Christos Pazis ameshirikiana na Merkouri inaitwa "Argises"

Merkouri alimaliza mwaka 2007 akiwa ametoa wimbo ulioko kwenye CD ukiitwa "Nai" (Ndio). Ilikuwa na nyimbo mbili "Nai" na "Kane Ena Tsigaro". "Nai" ulitengenezwa kipande cha video, na wimbo ulifika nafasi ya pili kwenye chati za nyimbo za IFPI kwa Ugiriki.

Muda mfupi baadae, Merkouri alirekodi albamu kwenye studio za Sony BMG Greece. Baada ya kutofautiana ndani na Sony BMG, Merkouri alitoa taarifa kukatisha mahusiano na lebo mnamo 2009, na haijulikani nini kitakachotokea na kazi ambazo hazikutolewa. Merkori alisaini na lebo mpya iliyoanzishwa E.DI.EL mnamo 2009, ambayo baadae ilibadilisha jina na kuwa 4Music. Mnamo katikati mwa 2009 Merkouri kidigitali aliachia wimbo "Parakseno Agori".

Diskographia

hariri

Albamu

hariri
  • 2002: Na Fysai I Anixi
  • 2003: Mine Mazi Mou Apopse
  • 2004: Palirroia
  • 2005: Aneta
  • 2006: Argises

Nyimbo za CD

hariri
  • 2007: "Nai"

Viungo vya nje

hariri

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Irini Merkouri kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.