Istilahi
Istilahi (kutoka Kiar. اصطلاح, Kiing. term, terminology) ni neno ambalo linawakilisha dhana fulani katika fani maalumu ya elimu kama vile siasa, sayansi, uchumi, ufundi, dini au hisabati. Ni pia elimu inayochunguza matumizi ya istilahi.
Istilahi za fani mbalimbali hutajwa kwa kutumia maneno ambayo yanaweza kuwa na maana tofauti katika lugha ya kila siku au katika kawaida ya fani nyingine.
Viungo vya Nje
hariri- Arnold B. G. Msigwa : Changamoto za Istilahi katika Uandishi wa Tasinifu za Uzamili wa Kiswahili Tanzania, jarida la Kiswahili, Vol. 79 No. 1 (2016), eISSN: 0023-1886
- S.S. SEWANGI: Uundaji wa Istilahi za Kiswahili Kileksikografia na Athari zake Archived 7 Oktoba 2021 at the Wayback Machine., Nordic Journal of African Studies 16(3): 333–344 (2007)
- E. Rukiramakuba: Vipengele Vya Kimsamiati Katika Kamusi Ya Kiswahili Sanifu, Dhima ya kamusi katika kusanifisha lugha (Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, 1995