Itumba ni kata ya Wilaya ya Ileje na ndiyo makao makuu ya wilaya hiyo. Imepakana na Isongole ambayo imepakana na nchi ya Malawi katika Mkoa wa Songwe, Tanzania. Msimbo wa posta ni 53401.

Kata ya Itumba
Nchi Tanzania
Mkoa Mkoa wa Songwe
Wilaya Ileje
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 10,566

Jina linatokana na tumbaku kwa lugha ya Kilambya. Hii ni kwa sababu mtawala mkuu wa Walambya alikuwa analima tumbaku pembezoni mwa mto Itumba, nayo ilikuwa inastawi sana pembezoni mwa mto huo.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 10,566 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata hii ilikuwa na wakazi wapatao 10,186 [2] walioishi humo.

Marejeo hariri

  1. https://www.nbs.go.tz, uk 235
  2. "Sensa ya 2012, Mbeya - Ileje DC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-13. 
  Kata za Wilaya ya Ileje - Mkoa wa Songwe - Tanzania  

Bupigu | Chitete | Ibaba | Ikinga | Isongole | Itale | Itumba | Kafule | Kalembo | Lubanda | Luswisi | Malangali | Mbebe | Mlale | Ndola | Ngulilo | Ngulugulu | Sange |


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Songwe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Itumba (Ileje) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari .
Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno