Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiarmenia

Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiarmenia Kiarmenia: Հայկական Սովետական Սոցիալիստական Հանրապետություն, Hajkakan Sowetakan Sozialistakan Hanrapetut'jun; Kirusi Армянская Социалистическая Советская Республика, Armjanskaja Sozialistitscheskaja Sowjetskaja Respublika) ilikuwa jina la Armenia ya leo ilipokuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti kati ya 1922 hadi 1991.

Bendera ya Armenia ya Kisovyeti
Nembo la Armenia ya Kisovyeti

Armenia na mauaji nchini Uturuki

hariri

Kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Armenia ilkuwa eneo kubwa zaidi kushinda leo lakini hapakuwa na dola la Armenia. Eneo la Waarmenia liligawiwa kati ya Uturuki na Urusi. Walio wengi waliishi upande wa Uturuki. Sehemu za mashariki za Armenia zilikuwa upande wa Urusi. Wakati wa vita kulitokea mauaji ya Waarmenia milioni 1.5 upande wa Uturuki. Wakimbizi wengi walijaribu kukimbilia pande za Kirusi za Armenia.

Armenia ya Kirusi kuwa nchi huria

hariri

Mwisho wa vita Milki ya Urusi iliporomoka kutokana na mapinduzi ya kibolsheviki na nchi za Kaukazi ya Kirusi zilitangaza uhuru pamoja na Armenia ya Kirusi tarehe 28 Mei 1918.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Armenia ikajikuta kati ya pande mbili: kwa upande moja ilikuwa katika hali ya vita na Uturuki ambako Waarmenia wengi walichinjwa na kufukuzwa na kwa upande mwingine jeshi la mapinduziya kibolsheviki lililojaribu kurudisha nutawala wake katika Kaukazi. Nchi yenyewe ilijaa wakimbizi ikapambana na matatizo ya vita, njaa na magonjwa. Armenia ya magharibi ilipotea wakati ule hakuna Waarmenia waliobaki upande wa Uturuki.

Mapinduzi ya Kibolsheviki na kuingizwa katika Umoja wa Kisovyeti

hariri

Mwaka 1920 Jamhuri ikaingiliwa na Wabolsheviki waliopindua serikali na kuchukua utawala.

Sehemu ya Shirikisho la Jamhuri ya Ng'ambo ya Kaukazi

hariri

Mwaka 1922 serikali ya Kibolsheviki ikaingiza Armenia katika Umoja wa Kisovyeti. Jamhuri ya Armenia ikaungwa pamoja na Georgia na Azerbaijan katika "Shirikisho la Jamhuri ya Ng'ambo ya Kaukazi" lililokuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti. Shirikisho hili likaondolewa tena 1936 na kila sehemu kuwa jamhuri iliyopo moja kwa moja chini ya Umoja wa Kisovyeti.

Mabadiliko chini ya udikteta wa Stalin

hariri

Chini ya udikteta wa Josef Stalin Waarmenia wliteswa kama watu wengine katiia Umoja wa Kisovyeti. Wabolsheviki walijaribu kuharibu kanisa. Katholikos (askofu mkuu) Choren I wa Erivan aliuawa usiku wa 5 Aprili 1938. Kati ya mapadre 1115 waliowahi kuwepo mwaka 1920 walibaki 12 pekee. Kati ya makanisa 850 yote yalifungwa isipokuwa 4.

Wasomi wengi waliuawa au kupelekwa katika makambi ya GULAG huko Siberia.

Waarmenia kama wengine walifaidika na kulegea kwa ukali wa udikteta baada ya Stalin. Lakini siasa ya kuitolea kipaumbele lugha ya Kirusi iliacha alama zake katikautamaduni wa kila siku na lugha ya Kiarmenia yenyewe.

Uhuru 1991

hariri

Kuporomoka kwa utawala wa kikomunisti tangu 1990 kuliwezesha uchaguzi huru katika mwezi wa Mei. Wapanzani walishinda. Harakati ya kudai uhuru wa nchi ikapewa mkasi. Bunge liliamua 23 Agosti 1991 kubadilisha jina la nchi kuwa "Jamhuri ya Armenia" (Հայաստանի Հանրապետություն - Hajastani Hanrapetut'jun).

Katika kura walimoshiriki 95% za wananchi wote kulitokea azimo la kujitenga na Umoja wa Kisovyeti (94,39% kura za "ndiyo"). Uhuri ikatangazwa tar. 30 Agosti 1991.