January Makamba (alizaliwa 28 Januari 1974) ni mwanasiasa na Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi. Anawakilisha Jimbo la Bumbuli, katika wilaya ya Lushoto, mkoa wa Tanga.

Januari Makamba mwaka 2012.

Alifaulu katika uchaguzi mkuu wa tarehe 31 Oktoba 2010 bila mpinzani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi. Mwaka 2015 alijaribu kupata nafasi ya mgombea wa urais kwa chama cha CCM [1]. Alirudi kwenye bunge 2015 na 2020 tena bila kuchaguliwa akiwa mgombea pekee.

Chini ya rais John Pombe Magufuli aliwahi kuwa Waziri wa Mazingira (2016-2019). Mwaka 2021 alipata kuwa waziri wa nishati katika baraza la mawaziri chini ya rais Samia Suluhu Hassan[2].

Marejeo

  1. http://taifaletu.blogspot.com/2015/06/hotuba-ya-january-makamba-ya-kutangaza.html Hotuba ya January Makamba ya kutangaza kuomba nafasi ya Urais wa Tanzania, Juni 7, 2015.
  2. https://greenwavesmedia.co.tz/sw/2021/09/makamba-aanza-kazi-rasmi-wizara-ya-nishati/ MAKAMBA AANZA KAZI RASMI WIZARA YA NISHATI, greenwavesmedia 13 Septemba 2021

Viungo vya nje

 
WikiMedia Commons