Jimbo la Mataifa ya Kusini, Ethiopia

Jimbo la Mataifa ya Kusini (Kiamhari: ደቡብ ብሔሮች ብሔረሰቦችና ሕዝቦች, Ye-Debub Bəheročč Bəheresebočč-ənna Həzbočč, Ing. "Southern Nations, Nationalities, and Peoples’ Region" SNNPR) ni moja ya majimbo 9 ya kujitawala ya Ethiopia.

Mji mkuu wa jimbo ni Awassa.Jimbo liko katika kusini ya nchi likipakana na Kenya upande wa kusini, Sudan upande wa magharibi na majimbo ya Ethiopia ya Gambela upande wa kaskazini na Oromia upande wa kaskazini, mashariki na kusini-mashariki.

Tofauti na majimbo mengine ya Ethiopia yenye kabila au kundi 1 hasa hapa kuna vikundi vingi vidogo-vidogo kwa jumla 45. Wakazi wengi huishi mashambani ama vijijini au kama wahamiaji katika makambi yao ya kuhama.


 
Majimbo ya Ethiopia
Bandera ya Ethiopia
Addis Abeba | Afar | Amhara | Benishangul-Gumuz | Dire Dawa | Gambela | Harar | Oromia | Somali | Mataifa ya Kusini | Tigray