Addis Ababa

(Elekezwa kutoka Addis Abeba)

Addis Ababa (pia Addis Abeba; kwa Kiamhara አዲስ አበባ, "Ua Jipya"; kwa Kioromo Finfinne) ni mji mkuu wa Ethiopia na wa Umoja wa Afrika.

Jiji la Addis Ababa


Jiji la Addis Ababa
Jiji la Addis Ababa is located in Ethiopia
Jiji la Addis Ababa
Jiji la Addis Ababa

Mahali pa mji wa Addis Ababa katika Ethiopia

Majiranukta: 9°1′48″N 38°44′24″E / 9.03000°N 38.74000°E / 9.03000; 38.74000
Nchi Ethiopia
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 3,352,000
Tovuti:  www.addisababacity.gov.et
Ramani ya Ethiopia ikionyesha Addis Ababa ilipo.
Addis Ababa, inavyoonekana kutoka angani.
Zaidi ya asilimia 51 ni wanawake.

Ina hadhi ya mji wa kujitawala (ras gez astedader) kama jimbo la Ethiopia.

Mji wenyewe una watu kutoka makabila 80, wakiongea lugha 80, na jamii za Waislamu na Wakristo.

Addis Ababa iko mita 2,500 juu ya usawa wa bahari kwa 9.03° N 38.74° E). [1]

Mwaka 2016, idadi ya wakazi ilikuwa 3,352,000 [2], na kwa hiyo Addis Ababa ndio mji mkubwa nchini.

Eneo hii lilichaguliwa na Malkia Taytu Betul na mji kuanzishwa mwaka wa 1886 na mume wake, Mfalme Menelik II, na sasa mji huu una umma milioni nne, na asilimia nane ya ukuzi wa uchumi.

Mji huu uko kwenye Mlima Entoto na ni makazi maalum ya Chuo Kikuu cha Addis Ababa. Chuo Kikuu cha Addis Ababa kilijulikana kama Chuo Kikuu cha Haile Selassie I, kutokana na jina la Mfalme wa mwisho wa Ethiopia, ambaye alitoa jumba la mfalme (Jumba Guenete Leul) liwe makao maalum ya Chuo Kikuu cha Addis Ababa mwaka wa 1961.

Historia

hariri

Addis Ababa ilianzishwa na Mfalme wa Ethiopia Menelik II. Menelik, kama mfalme wa Shewa, aligundua mlima Entoto kama kambi nzuri sana ya jeshi ili kumiliki upande wa kusini, na mwaka wa 1879 alitembea kwa mibomoko ya kale ya mji huu, na kuona kanisa ambalo ujenzi haukuwa umemalizwa, kuthibati kuwa Waethiopia waliishi katika mji huu kabla ya vita za Ahmad Gragn.

Masilahi ya Menelik wa pili yaliongezeka, mke wake alipoanza kazi ya ujenzi wa kanisa eneo la Entoto, na Menelik kuamrisha kanisa la pili eneo hilo. Lakini eneo hilo halikutua kuwa mji haraka kwa sababu ya ukosefu wa kuni na maji, na makazi hasa yalianzia katika bonde kusini mwa mlima mwaka wa 1886.

Mwanzo, Malkia Taytu alijijengea nyumba karibu na "Filwoha", chemchem moto iliyo na madini, ambayo yajulikana na wenyeji Waoromo kama Finfinne, Malkia Taytu na watumishi Washowan wa kifalme walipenda sana kuoga kwa maji hayo yaliyo na madini. Washarifu wengine na watumishi na mali yao, wao pia walikaa sehemu hii, na Menelik kuongeza jumba la mke wake, ili iwe Jumba Rasmi la Miliki ambayo ndio makazi rasmi ya serikali Addis Ababa mpaka leo.

Menelik wa pili kaanza Addis Ababa kama Mji Mkuu wa Ethiopia. Mojawapo ya maendeleo Menelik alifanya ni kama kupanda miti ya mkaratusi kwa mitaa kando ya barabara.

Mwaka wa 1936, jeshi la Waitalia lilitwaa Addis Ababa kwa Vita vya Pili vya Italia na Uhabeshi, na kuifanya mji mkuu wa Afrika Mashariki ya Kiitalia. Addis Ababa iliongozwa na gavana kutoka mwaka wa 1936 mpaka 1939.

Baadaye Waitalia walipingwa na wazalendo wa Ethiopia na pia kushindwa vitani na Waethiopia kwa usaidizi wa Waingereza katika kampeni ya Afrika Mashariki na pia ukombozi wa Ethiopia, Mfalme Haile Selassie alirudi Addis Ababa tarehe 5 Mei 1941, baada ya miaka mitano kamili, na kuanza kazi ya kuendeleza mji mkuu wake.

Mfalme Haile Selassie alisaidia kuanzisha Organizesheni ya Umoja wa Afrika mwaka 1963 akaikaribisha kuwa na makao makuu mjini. Ilipogeuka kuwa Umoja wa Afrika mwaka 2002, makao yakabaki yaleyale.

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. "World-Gazeteer". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-03-25. Iliwekwa mnamo 2006-05-14.
  2. "World-Gazeteer". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-10-01. Iliwekwa mnamo 2006-05-14.

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


 
Majimbo ya Ethiopia
 
Addis Abeba | Afar | Amhara | Benishangul-Gumuz | Dire Dawa | Gambela | Harar | Oromia | Sidama | Somali | Mataifa ya Kusini | Tigray