Majimbo ya Ethiopia

Majimbo ya Ethiopia ni vitengo vikuu vya kujitawala chini ya ngazi ya kitaifa katika muundo wa shirikisho la Ethiopia.

Kuna majimbo 9 yanayogawiwa kwa msingi wa lugha kuu zinazojadiliwa katika jimbo pamoja na majiji 2 yenye hadhi ya jimbo (astedader akababiwach, umoja: astedader akabibi) ambayo ni Addis Ababa na Dire Dawa.

Hii ni orodha ya Majimbo (wingi - kililoch; umoja – kilil) ya Ethiopia:

OrodhaEdit

Ramani A-Z Jimbo Mji mkuu Eneo (km²) Wakazi (2005) Lugha kuu za jimbo
 
1 Addis Abeba Addis Abeba 530 3.627.934 --
2   Afar Asayita 96.707 1.389.004 Kiafar
3   Amhara Bahir Dar 159.174 19.120.005 Kiamhara
4   Benishangul-Gumuz Asosa 49.289 align=center Berta, Gumuz
5 Dire Dawa Dire Dawa 1.213 398.934 Kioromo, Kiamhara, Kisomali
6   Gambela Gambela 25.802 247.000 Nuer, Anuak
7   Harari Harar 374 196.000 Aderi; Oromo, Somali
8   Oromia Adama 353.362 25.125.000 Oromo
9   Somali Jijiga 279.252 4.329.000 Kisomali
10   Mataifa ya Kusini Awasa 112.343 14.901.990 Sidama, Wolaytta, Hadiyya, Gurage na vingine
11   Tigray Mekele 50.078 4.334.996 Kitigray

Tazama piaEdit


 
Majimbo ya Ethiopia
 
Addis Abeba | Afar | Amhara | Benishangul-Gumuz | Dire Dawa | Gambela | Harar | Oromia | Somali | Mataifa ya Kusini | Tigray