Jiolojia
Jiolojia (kutoka Kigiriki γῆ ge „ardhi“ na λόγος logos, somo, mafundisho“ = "geologia" - kwa matamshi ya Kiingereza "jiolojia") ni fani ya sayansi inayochunguza maumbile ya dunia na tabia zake za kifizikia na kikemia. Inachungulia pia historia ya dunia na nguvu zinazoendelea kubadilisha maumbile ya dunia.
Neno "geologia" liliwahi kutumiwa mara ya kwanza mnamo 1778 na Mfaransa Jean-André Deluc (1727–1817).
Jiolojia inatazama mawe na ardhi ikitafuta maelezo kwa umbo na tabia zake kuligana na kanuni za kisayansi.
Kuna masomo madogo ndani ya jiolojia kama vile:
- Petrolojia ni elimu ya mawe na miamba
- Mineralojia ni elimu ya madini
- Jiolojia ya kihistoria ni elimu ya matokeo yaliyosababisha kutokea kwa mawe, miamba, milima na mabara jinsi yalivyo leo
- Paleontolojia ni elimu ya visukuku (mabaki ya miili ya wanyama wa kale yaliyokuwa kama mwamba)
- Hidrojiolojia ni elimu ya hali ya maji chini ya uso wa dunia
- Volkenolojia ni elimu ya volkeno kwenye mabara au chini ya bahari
Aina za miamba
haririJiolojia inachunguza hasa miamba na kutofautisha aina tatu kufuatana na misingi yake:
- Mwamba Moto: mwamba wa mgando au mwamba wa kivolkeno unajitokeza pale ambako magma au zaha (lava) inaganda.
- Mwamba Tabaka: mwamba mashapo hutokea pale ambako miamba inavunjika na kusagwa katika mmomonyoko na mashapo yanakandamizwa kwa njia ya kanieneo ya mashapo ya juu hadi mashapo kuwa mwamba mapya.
- Mwamba Geu: mwamba metamofia ni mageuzi ya miamba ya awali -ama ya kivolkeno au ya mishapo- kwa njia ya kanieneo kubwa sana na joto kali kuwa aina mpya ya mwamba. Metamofosi kwa kawaida hutokea katika kina kubwa.
Ardhi
haririAsili ya ardhi ni miamba iliyovunjikavunjika na kuchanganyika na mabaki ya mimea na wanyama waliooza.
Picha
hariri-
Maganda ya mwamba mashapo
-
Maganda ya mwamba mashapo yamekatika
-
Mwamba mashapo uliotokea kutokana na vipande vyeupe vya mwamba wa kale uliovunjika na kuchnganyika na mchanga mwekundu kwenye mlalo wa mtoni
-
"Zimbabwe Great Dyke": Kanda la mwamba wa kivolkeno unakata mwamba wa mashapo. Picha kutoka chombo cha angani.
-
Ufukwe ni mahali pazuri kwa kazi ya mwanajiolojia
-
....mapango vilevile.
-
Uso huu wa mwamba unamsimulia mwanajiolojia historia yake.
-
Uso huu wa mwaba nchini Ufaransa huonyesha madini ya mica.
-
Nyundo kama hii ni chombo muhimu cha mwanajiolojia.
-
Wanajiolojia hutumia kekee kama hii kutoboa mashimo na kutoa sampuli za mwaba kutoka chini ya uso wa ardhi.
-
Sanduku hii inajaa sampuli ya miamba zilizotolewa ardhini kwa kekee.
-
Wanajiolojia hutazama mwamba wakitafuta madini.
-
Ramani inaoyonyesha aina za ardhi na mwamba chini ya Bahari ya Kusini.
-
Ramani ya mabamba ya gandunia.
-
Diageramu juu ya mlipuko wa volkeno chini ya bahari.
Viungo vya nje
hariri- https://www.youtube.com/watch?v=RUwS1uAdUcI
- One Geology: Ramani ya jiolojia iliyozinduliwa mwaka 2007 ikawa moja ya mchango wa 'Mwaka wa Kimataifa wa Sayari ya Dunia'.
- Habari, Tamani, Kamusi, Makala, Kazi
- American Geophysical Union
- American Geosciences Institute
- European Geosciences Union
- Geological Society of America Ilihifadhiwa 29 Oktoba 2011 kwenye Wayback Machine.
- Geological Society of London
- Video za mahojiano na wanajiolojia maarufu duniani
- Geology OpenTextbook