Jiriwa
Jiriwa (kwa Kiingereza: vise au vice) ni kibanio cha chuma au mbao ambacho hushikilia vitu kwa imara wakati vinapofanyiwa kazi.
Huwa na mikono miwili, mmoja uliosanikishwa na mwingine unaoweza kusogezwa kwa njia ya parafujo ya kukaza au wenzo wa kubana.
Aina tofautiEdit
Jiriwa ya seremalaEdit
Jiriwa huunganishwa katika meza ya seremala, kwa kawaida sawa na uso wa meza. Mikono yake ni ama ya mbao ama ya chuma; kama ni chuma kinafunikwa kwa mbao ili kutoacha alama kwenye vipande vinavyoshikwa.[1]
Jiriwa ya fundi vyumaEdit
Jiriwa ya fundi vyuma hutumiwa kushika metali, si mbao, wakati wa kukata au kupiga tupa.
Jiriwa hiyo kwa kawaida hufungwa kwa skrubu juu ya uso wa meza ya fundi. Mara nyingi huwa na sehemu ndogo ya fuawe. Kwa kawaida hukaa juu ya kiti chenye mhimili wa kuzunguka kinachorahisisha kufanya kazi pande zote.
Jiriwa ya fundi bombaEdit
Fundi bomba huhitaji jiriwa yenye mikono inayoshika bomba kirahisi, wakati anapokata hesi.
MarejeoEdit
- ↑ Bentzley, Craig (2011). "Installing a Bench Vise". Woodcraft Magazine (June/July): 50–53. http://www.woodcraftmagazine.com/onlineextras/41-Vises.pdf.