Joyce Lazaro Ndalichako

Mwanasiasa wa Tanzania

Joyce Lazaro Ndalichako (alizaliwa Musoma, 21 Mei 1964) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa Chama cha kisiasa cha CCM. Aliteuliwa[1] na Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kuwa mbunge na pia Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kwa miaka 20152020 nchini Tanzania[2] akiendelea hata katika awamu ya sita chini ya Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Prof Joyce Ndalichako Mb

Waziri wa elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi
Aliingia ofisini 
2015
Rais John Magufuli
aliyemfuata Shukuru Kawambwa

Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
Muda wa Utawala
2005 – 2014
mtangulizi Dr Charles Msonde

Mbunge
Muda wa Utawala
2015 – 2020
Appointed by John Magufuli
Constituency Hana jimbo (Mbunge wa viti maalam)

tarehe ya kuzaliwa 21 Mei 1964
Musoma, Mara
utaifa Mtanzania
chama CCM (1982–sasa)
mhitimu wa University of Dar Es Salaam (B.Sc. with Education), University of Alberta (PhD)
dini Mkristo
Joyce Ndalichako, wa pili kutoka kushoto

Elimu yake

hariri

Joyce Ndalichako alipata shahada yake ya kwanza katika Ualimu (kwa Kiingereza: Bachelor of Science with Education, majoring in Mathematics), akijikita katika Hisabati, katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania mnamo mwaka 1987 hadi 1991. Alipata shahada yake ya Uzamivu katika Saikolojia ya Elimu (Kiingereza: PhD in Educational Pyschology, major in Educational Statistics & Measurement and Evaluation), akijikita katika Takwimu za Kielimu na Vipimo vya Kielimu pamoja na Tathmini ya Elimu, katika Chuo Kikuu cha Alberta nchini Kanada. [3]

Kazi yake

hariri
  • Mnamo mwaka 2000 hadi 2005, Joyce Ndalichako alikuwa ni mhadhiri mkuu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akifundisha masuala ya Vipimo vya Kielimu na Tathmini ya Elimu, mbinu za Utafiti na Takwimu za Kielimu, huku akisimamia kazi (Kiingereza: dissertation) za wanafunzi wake.[4][3]
  • Kuanzia mwaka 2014 hadi leo, Joyce Ndalichako ni profesa msaidizi na mkuu msaidizi kwa upande wa Utafiti katika Chuo Kikuu cha Agha Khan, Taasisi ya Maendeleo ya Elimu, Afrika Mashariki.[3][4]

Marejeo

hariri
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-12-25. Iliwekwa mnamo 2017-05-13.
  2. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017
  3. 3.0 3.1 3.2 "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-07-25. Iliwekwa mnamo 2020-07-25.
  4. 4.0 4.1 "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-08-19. Iliwekwa mnamo 2020-07-25.