Katika utarakilishi , kumbukizi soma tu (kwa kifupi: KUSOTU; kwa Kiingereza: Read-only memory au ROM) ni aina ya kumbukizi (kwa usahihi zaidi, kumbukizi si-fukivu) inayotumika kwenye tarakilishi na mashine nyingine ya kielectroniki.

Picha ya KUSOTU.

Data za KUSOTU haziwezi kubadilika baada ya utengenezaji wa kifaa cha kutunzia hiki. Hivyo KUSOTU inatumika kutunzia data za programu zinazobadilika kwa nadra.

MarejeoEdit

  • Kiputiputi, O. (2011). Kamusi sanifu ya kompyuta. Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, K.602.