Gaius Messius Quintus Traianus Decius (takriban 201 – Juni 251) alikuwa Kaizari wa Dola la Roma kuanzia Septemba 249 hadi kifo chake.

Shaba inayoonyesha Kaizari Decius

Alimfuata Philippus Mwarabu kwa kumshinda katika pigano la vita na kumuua. Baadaye alitawala pamoja na mwana wake Herennius Etruscus.

Mnamo mwaka 250 aliagiza ibada zitekelezwe na raia wote wakitakiwa kutoa sadaka mbele ya sanamu za miungu. Kwa njia hiyo alisababisha mateso ya Wakristo wengi waliokataa kutoa sadaka hizo.

Tazama pia

hariri
  Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Roma bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kaizari Decius kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.