Kaluta Amri Abeid
Shekhe Kaluta Amri Abeid (mkoa wa Kigoma, 1924 [1] - 1 Januari 1964) alikuwa meya wa kwanza Mwafrika [2] na mwanasiasa pamoja na mhubiri wa dini.
Kwa jina la utani la kishairi alikuwa akijulikana kama Adili, lakini katika kipindi cha utoto wake baba yake alipenda kumuita kwa jina la Simba wa Lumona [3][4], kama ilivyo kwa washairi wengi kutumia majina ya utani au lakabu.
Baba yake alijulikana kama Abeid Kaluta na mama yake alijulikana kama Joha Kakolwa,
Uwanja maarufu wa mpira katika mkoa wa Arusha hujulikana kama uwanja wa kumbukumbu wa Shekhe Amri Abeid, ni uwanja ulopewa jina la mwanasiasa na mshairi huyu mkubwa nchini Tanzania [5].
Tanbihi
hariri- ↑ Tarehe rasmi na mwezi wa kuzaliwa vimekuwa havijulikani kutokana na kutokutunzwa vyema kwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwake
- ↑ Maina, Stephen. "Mwalimu J.K.Nyerere na Kaluta Amri Abeid". Mwananchi. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-01-27. Iliwekwa mnamo 2020-01-27.
Kaluta Amri Abeid alizaliwa Ujiji Kigoma mwaka 1924. Alikuwa ni mtoto wa pili wa kiume katika familia ya watoto kumi. Mwaka 1930 alianza masomo ya madrasa kwa miaka mitatu na baadaye kujiunga na shule ya msingi. Alijiunga na shule ya Sekondari ya Tabora na baadaye alisomea ukarani hapa Dar es Salaam mwaka 1942 – 1943.
- ↑ Simba wa Lumona ni jina linalotokana na mtemi maarufu aliyekuwepo katika nchi ya Congo na aliyetokana na vizazi vya Pole
- ↑ ISBN 978-9987-9650-2-1
- ↑ "Hivi viwanja vione tu, ni majina ya watu na mitaa". Mwanaspoti (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-01-27. Iliwekwa mnamo 2020-01-27.
Viungo vya nje
hariri- Shairi la Kaluta Amri Abedi - Sumu Ya Ua katika YouTube. Muda wa video dakika 3 sekunde 53. Mpakiaji: SheikhBakri AbediKaluta, 2015.
Makala hiyo kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |