Kampuni ya Magazeti ya Bay State
Kampuni ya Magazeti ya Bay State ina makao yake makuu Somerville, Massachusetts, Marekani.
Kampuni ya Magazeti ya Bay State | |
---|---|
Jina la kampuni | Kampuni ya Magazeti ya Bay State |
Ilianzishwa | 1 Mei 1991 |
Mwanzilishi | *. William P. Dole(mmiliki wa hapo awali) |
Huduma zinazowasilishwa | Uchapishaji |
Mmiliki | Fidelity Investments |
Makao Makuu ya kampuni | *. Somerville *. Massachusetts |
Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii | Magazeti ya Kila Wiki |
Nchi | Marekani |
Historia
haririIlikuwa kampuni ya uchapishaji ya magazeti ya kila wiki katika maeneo kaskazini mwa Boston. Iliundwa katika mwaka wa 1991 na kampuni ya Fidelity Investments baada ya kununua kampuni ya Dole Publishing kutoka mmiliki wake wa muda mrefu, William P. Dole.
Kampuni ya Magazeti ya Bay State ilifungwa na kuwekwa katika kitengo cha Metro cha Kampuni ya Magazeti ya Community inayomilikiwa na Fidelity katika mwaka wa 1996. Kampuni ya Magazeti ya Community hivi sasa inamilikiwa na GateHouse Media.
Mali za Bay State zilikusanywa na familia ya Dole, iliyoendesha gazeti la Cambridge Chronicle tangu miaka ya 1930 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 1990. Gazeti la Chronicle, gazeti la kuchapisha rekodi za jiji la Cambridge, limechapishwa tangu mwaka wa 1846 na, chini ya usimamizi wa familia ya Dole, likaungana na gazeti shindani la Cambridge Sun.
Familia ya Dole ilinunua pia magazeti makuu ya kila wiki katika miji mingine miwili kaskazini mwa Boston na vilevile kuchapisha majarida mengine mbalimbali.
Mali
haririWakati wa ununuzi na Fidelity katika mwaka wa 1991, kampuni ya uchapishaji ya Dole (ilibadlishwa jina kuwa Kampuni ya Magazeti ya Bay State) ilihusisha magazeti matatu ya kila wiki, yote yakipatikana katika kata ya Middlesex, Massachusetts.
- Cambridge Chronicle ya Cambridge (ilianzishwa mwaka wa 1846)
- Somerville Journal ya Somerville
- Watertown Press ya Watertown
Magazeti haya yote bado huchapishwa chini ya Kitengo cha Metro cha Kampuni ya Magazeti ya Community. Kampuni ya Bay State ilichapisha jarida dogo la wanunuzi katika eneo la Lowell, chapisho hilo liliitwa Merrimack Valley Advertiser. Chapisho hilo lilibadilishwa baadaye kuwa majarida mawili ya Advertiser katika Tewksbury na Wilmington, haya yanachapishwa, hivi sasa, na Kitengo cha Kaskazini Magharibi chini ya majina ya Tewksbury Advocate na The Wilmington Advocate.
Angalia pia
haririMarejeo
hariri- "Dole Publishing Is Sold". The Boston Globe, 19 Aprili 1991.
- [1]
Viungo vya nje
hariri- Tovuti ya GateHouse Media
- Kampuni ya gazeti la Jimbo la Bay Bay GoToPublish
- Wasifu wa CNC Ilihifadhiwa 31 Agosti 2010 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kampuni ya Magazeti ya Bay State kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |