Kanisa la Kitume la Armenia

Kanisa la Kitume la Armenia (kwa Kiarmenia: Հայ Առաքելական Եկեղեցի), ambalo pengine linaitwa pia Kanisa la Kiorthodoksi la Armenia au Kanisa la Kigregori, ni Kanisa la kitaifa la kale zaidi duniani (301).

Ubatizo wa mfalme Tiridate III ulioingiza taifa la Armenia katika Ukristo.

Wafuasi wake wanahesabiwa kati ya Waorthodoksi wa Mashariki kwa sababu hawakubali Mtaguso wa Kalsedonia na Mitaguso ya kiekumeni iliyofuata.

Upande wa ibada, linatumia liturujia ya Armenia.

Uongozi na uenezi

hariri

Mkuu wake anaitwa Catholikos (kwa Waarmenia cheo hicho ni cha juu kuliko kile cha "Patriarki") na makao yake makuu yako katika mji wa Echmiadzin, huko Armenia. Kwa sasa ni Karekin II.

Yupo pia Catholikos mwingine mwenye makao makuu Antilyas huko Lebanoni. Kwa sasa ni Aram I.

Kutoka huko wanaongoza Waarmenia milioni 7 hivi waliosambaa duniani hasa baada ya maangamizi ya halaiki yaliyofanywa na Waturuki baada ya Vita Vikuu vya kwanza.

Viungo vya nje

hariri