Liturujia ya Armenia
Liturujia ya Armenia ni liturujia maalumu ya Ukristo ambayo leo inatumiwa na Kanisa la Mitume la Armenia na vilevile na Kanisa Katoliki la Armenia kokote duniani.
Liturujia hiyo inafuata mapokeo ya Gregori Mletamwanga, mwanzilishi na msimamizi wa Kanisa huko Armenia.
Majengo
haririMakanisa ya Kiarmenia kwa kawaida yana mapazia yanayotenganisha padri altareni na walei washiriki wakati wa sehemu fulanifulani za ibada, lakini si ukuta wa picha takatifu unaopatikana katika Makanisa ya Kiorthodoksi.
Athari za liturujia nyingine
haririDaima liturujia hiyo imekuwa tayari kuathiriwa na madhehebu mengine. Kwa mfano, maaskofu wanavaa kichwani mitra kama wale wa Kanisa la Kilatini.
Pia unatumika mkate usiotiwa chachu kwa ajili ya ekaristi.
Kumbe ni jambo la pekee kutochanganya maji kidogo katika divai kama ilivyo desturi ya madhehebu mengine.
Kati ya anafora zote za Kiarmenia, kuanzia karne ya 10 inatumika ile tu inayoitwa ya Atanasi wa Aleksandria iliyotafsiriwa kutoka Kigiriki.
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- New Catholic Dictionary: Armenian Rite Archived 16 Juni 2006 at the Wayback Machine.
- Misa ya Kiarmenia ya Kikatoliki Archived 2 Novemba 2007 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Liturujia ya Armenia kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |