Kanuni ya Imani ya Mitume


Kanuni ya Imani ya Mitume (kwa Kilatini: Symbolum Apostolorum au Symbolum Apostolicum) ni ungamo la imani ya Ukristo lililoanza kutumika mjini Roma katika karne ya 2 kwa ajili ya ubatizo, halafu likaenea hasa katika Kanisa la Magharibi.[1]

Mchoro wa karne ya 13 ukionyesha Thenashara wakiandika Kanuni ya Imani, ilivyosadikika wakati huo.

Kanuni hiyo inaendelea kutumiwa na Kanisa Katoliki na madhehebu mengi ya Uprotestanti katika liturujia na katekesi.

Kwa kuwa ilitokea Ulaya Magharibi, ambapo elekeo la kinadharia si kubwa kama huko Ugiriki, tena mapema kuliko mabishano mengi ya teolojia kuhusu umungu wa Yesu Kristo na wa Roho Mtakatifu, haina ufafanuzi wa kina.

Maandishi ya zamani zaidi tuliyonayo yanayoitaja "Kanuni ya Imani ya Mitume" ni barua ya mwaka 390 hivi kutoka sinodi ya Milano kwa Papa Siricius.[2][3][4]

Matini kwa KilatiniEdit

Credo in Deum Patrem omnipotentem, Creatorem caeli et terrae,
et in Iesum Christum, Filium Eius unicum, Dominum nostrum,
qui conceptus est de Spiritu Sancto, natus ex Maria Virgine,
passus sub Pontio Pilato, crucifixus, mortuus, et sepultus,
descendit ad inferos, tertia die resurrexit a mortuis,
ascendit ad caelos, sedet ad dexteram Patris omnipotentis,
inde venturus est iudicare vivos et mortuos.
Credo in Spiritum Sanctum,
sanctam Ecclesiam catholicam, sanctorum communionem,
remissionem peccatorum,
carnis resurrectionem,
vitam aeternam.
Amen.[5]

Tafsiri ya Kiswahili ya Kanisa Katoliki[6]Edit

Kwa Kiswahili, Kanisa Katoliki linatumia tafsiri hii:

Nasadiki kwa Mungu Baba mwenyezi, muumba wa mbingu na dunia,

na kwa Yesu Kristo, Mwanae pekee, Bwana wetu, aliyetungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria,

akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu.

Siku ya tatu akafufuka kutoka wafu, akapaa mbinguni, ameketi kuume kwa Mungu Baba mwenyezi; kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.

Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu katoliki, ushirika wa watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, na uzima wa milele. Amina.

Tafsiri ya Kiswahili ya WaprotestantiEdit

(kuna tofauti ndogo baina ya Walutheri na Wamoravian katika sehemu ya tatu)
Namwamini Mungu Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na nchi;

Na Yesu Kristo, Mwana wake pekee, Bwana wetu, aliyechukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Mariamu;
akateswa zamani za Pontio Pilato, akasulibiwa, akafa, akazikwa, akashuka kuzimu, siku ya tatu akafufuka kutoka kwa wafu, akapaa mbinguni;
ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba Mwenyezi, kutoka huku atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.

Namwamini Roho Mtakatifu,
Kanisa takatifu lililopo popote[7],
ushirika wa watakatifu,
ondoleo la dhambi,
kufufuliwa kwa mwili
na uzima wa milele.
Amin.

TanbihiEdit

  1. Neno la Kilatini symbolum, ishara, zawadi, linatokana na Kigiriki σύμβολον, kutoka kitenzi συμβάλλειν, kuweka pamoja, kulinganisha" (The American Heritage Dictionary of the English Language).
  2. Jack Rogers, Presbyterian Creeds (Westminster John Knox Press 1985 ISBN 978-0-664-25496-4), pp. 62–63
  3. James Orr: The Apostles' Creed, in International Standard Bible Encyclopedia. Reformed.org. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-06-22. Iliwekwa mnamo 2011-05-19.
  4. Apostles Creed. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-03-12. Iliwekwa mnamo 2014-09-21.
  5. Catechismus Catholicae Ecclesiae. Vatican.va (1992-06-25). Iliwekwa mnamo 2014-08-05.
  6. Misale ya Waamini, toleo la mwaka 2021, uk. 513
  7. Umbo la Walutheri: "lililo moja tu"

MarejeoEdit

  • Lochman, Jan Milič (1999), "Apostles' Creed", in Fahlbusch, Erwin, Encyclopedia of Christianity 1, Grand Rapids: Wm. B. Eerdmans, pp. 109–110, ISBN 0-8028-2413-7 
  • (2013) Rooted:The Apostles' Creed. Oro Valley, AZ: Doulos Resources. ISBN 978-1-937063-92-4. 

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kanuni ya Imani ya Mitume kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.