Katekesi
Katekesi (kutoka kitenzi cha Kigiriki κατηχεῖν, kateekhein, maana yake "kufundisha kwa sauti", ambacho ni mnyambuliko wa ἠχεῖν ("kufanya isikike") ni ufafanuzi wa mpango wa imani ya Ukristo.
Hatua ya katekesi inafuata ile ya awali ya kutangaza mbiu ya Injili kwa watu ili waone jinsi habari njema ya kifo na ufufuko wa Yesu ilivyo muhimu kwao, hasa upande wa wokovu.
Kwa kawaida kazi ya katekesi inaongoza waamini kwenye sakramenti mbalimbali, kuanzia ubatizo. Anayejiandaa kuupokea anaitwa mkatekumeni.
Katekista kwa kawaida anatumia kitabu rasmi maalumu kinachoitwa katekisimu, mbali ya Biblia ya Kikristo.
Ujumbe wenyewe unaeleweka kuwa hasa Injili kadiri ya imani ya Kanisa, yaani yale ambayo lenyewe "linaungama, linaadhimisha, linaishi na linasali kila siku" (Papa Yohane Paulo II).
Chuo cha katekesi cha kwanza kilianzishwa na Panteno huko Aleksandria (Misri) mwishoni mwa karne ya 2, kikapata sifa hasa chini ya uongozi wa waandamizi wake, Klemens wa Aleksandria na Origenes.
Mbali ya hiyo Shule ya Aleksandria, wakati wa mababu wa Kanisa ilikuwa maarufu vilevile Shule ya Antiokia (huko Siria, leo nchini Uturuki).
Marejeo
hariri- Green, Ian (1996). The Christian's ABC: Catechisms and Catechizing in England c.1530-1740. Oxford: Clarendon PressKigezo:Subscription required. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-01-08. Iliwekwa mnamo 2017-10-01.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help); Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - Luther, Martin; Theodore G. Tappert Ed. (1959). The Book of Concord the confessions of the Evangelical Lutheran Church. Luther's Small Catechism Art. i. Philadelphia: Mühlenberg Press. uk. 342.
In the Plain Form in Which the Head of the Family Shall Teach Them to His Household
- Manternach, Janaan; Pfeifer, Carl J. (1991). Creative catechist: a comprehensive, illustrated guide for training religion teachers (tol. la 2). Twenty-Third Publications. uk. 23. ISBN 978-0-89622-490-2. Iliwekwa mnamo 2010-11-06.
The life of the community and its diverse individuals now are seen as both the primary curriculum and the primary catechist.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Old, Hughes Oliphant (1992). The Shaping of the Reformed Baptismal Rite in the Sixteenth Century. Grand Rapids, MI: William B. Eerdmans Publishing Company. ISBN 978-0802824899.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help)
Viungo vya nje
hariri- Yohane Paulo II, hati Catechesi tradendae (1979)
- Course 'Catechism of the Catholic Doctrine' Archived 6 Julai 2017 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Katekesi kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |