Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli

Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli ni fomula rasmi ambayo ilipitishwa na Mtaguso wa kwanza wa Nisea (325)[1] ikakamilishwa na Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli (381) ili kubainisha imani sahihi ya Kanisa Katoliki dhidi ya uzushi, hasa wa Ario na wafuasi wake.

Nakala ya kale zaidi ya Kanuni ya Nisea, karne ya 5.
Picha takatifu ya karne ya 17 kutoka Urusi inayoonyesha mafundisho ya Nasadiki hiyo.

Katima mazingira hayo, lengo kuu lilikuwa kwanza kumkiri Yesu kama Mungu kweli sawa na Baba, halafu kwamba Roho Mtakatifu anastahili kuabudiwa pamoja na Baba na Mwana (Utatu Mtakatifu).

Hadi leo hiyo kanuni ya imani inatumika sana katika madhehebu mengi ya Ukristo, hata kama sehemu ya liturujia.[2][3][4][5][6][7][8][9]

Tafsiri ya KiswahiliEdit

Kwa Kiswahili, Kanisa Katoliki linatumia tafsiri hii:

Nasadiki kwa Mungu mmoja Baba mwenyezi, Muumba wa mbingu na dunia na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.

Nasadiki kwa Bwana mmoja, Yesu Kristo, Mwanae pekee wa Mungu, aliyezaliwa kwa Baba tangu milele yote. Mungu aliyetoka kwa Mungu, mwanga kwa mwanga, Mungu kweli kwa Mungu kweli, aliyezaliwa, bila kuumbwa, mwenye umungu mmoja na Baba: ambaye vitu vyote vimeumbwa naye.

Alishuka kutoka mbinguni, kwa ajili yetu sisi wanadamu, na kwa ajili ya wokovu wetu. Akatwaa mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kwake yeye Bikira Maria, akawa mwanadamu.

Akasulubiwa kwa ajili yetu sisi, kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato; akateswa, akafa, akazikwa, siku ya tatu akafufuka, kadiri ya Maandiko, akapaa mbinguni, amekaa kuume kwa Baba.

Atakuja tena kwa utukufu, kuwahukumu wazima na wafu, nao ufalme wake hautakuwa na mwisho.

Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Bwana mleta uzima: atokaye kwa Baba na Mwana.

Anayeabudiwa na kutukuzwa, pamoja na Baba na Mwana: aliyenena kwa vinywa vya manabii.

Nasadiki kwa Kanisa moja, takatifu, katoliki, la Mitume.

Naungama ubatizo mmoja kwa maondoleo ya dhambi.

Nangojea na ufufuko wa wafu,

na uzima wa milele ijayo. Amina.

Tofauti kati ya toleo la Nisea na lile la KonstantinopoliEdit

Tunaweza kulinganisha matoleo hayo mawili ya Kigiriki[10] kama ifuatavyo:

Mtaguso wa kwanza wa Nisea (325) Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli (381)
Lua error in Module:Unicode_data at line 293: attempt to index local 'data_module' (a boolean value). Lua error in Module:Unicode_data at line 293: attempt to index local 'data_module' (a boolean value).

Lua error in Module:Unicode_data at line 293: attempt to index local 'data_module' (a boolean value).

Suala la FilioqueEdit

Makala kuu: Filioque

Mwishoni mwa karne ya 6, baadhi ya makanisa ya Kilatini yaliongeza neno Filioque (na (kwa) Mwana) ambalo lilipingwa na Makanisa ya Kiorthodoksi kama upotoshaji wa imani juu ya mahusiano kati ya nafsi tatu za Mungu [11][12]

Idara husika ya Kanisa Katoliki huko Vatikano iliweka wazi mwaka 1995 kwamba, kama maneno ya Kigiriki καὶ τοῦ Υἱοῦ ("na kwa Mwana") yangeongezwa kwa ἐκπορεύομαι yangekuwa ya kizushi kweli[13][14][15] lakini neno Filioque si la kizushi likiongezwa kwa neno la Kilatini procedit kwa kuwa hilo si sawa na ἐκπόρευμαι[16][17]

TanbihiEdit

 1. Readings in the History of Christian Theology by William Carl Placher 1988 ISBN 0-664-24057-7 pages 52–53
 2. http://www.newadvent.org/cathen/04479a.htm
 3. Congregation for the Doctrine of the Faith, "Profession of Faith"
 4. Code of Canon Law, canon 833
 5. [1] "Archbishop Averky Liturgics – The Small Compline", Retrieved 2013-04-14
 6. [2] "Archbishop Averky Liturgics – The Symbol of Faith", Retrieved 2013-04-14
 7. Religion Facts, four of the five Protestant denominations studied agree with the Nicene Creed and the fifth may as well, they just don't do creeds in general. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-03-19. Iliwekwa mnamo October 29, 2014.
 8. Christianity Today reports on a study that shows most evangelicals believe the basic Nicene formulation. Iliwekwa mnamo October 29, 2014.
 9. Encyclopedia Britannica. Iliwekwa mnamo June 16, 2013.
 10. Symbolum Nicaeno-Constantinopolitanum – Greek
 11. Canon VII
 12. Kwa mtazamo tofauti, rejea Excursus on the Words πίστιν ἑτέραν
 13. http://biblehub.com/greek/1607.htm
 14. St. Gregory of Nazianzus, Oratio 39 in sancta lumina, in Patrologia Graeca, ed. by J.P. Migne, vol. 36, D’Ambroise, Paris 1858, XII, PG 36, 348 B: Πνεῦμα ἅγιον ἀληθῶς τὸ πνεῦμα, προϊὸν μὲν ἐκ τοῦ Πατρὸς, οὐχ ὑϊκῶς δὲ, οὐδὲ γὰρ γεννητῶς, ἀλλ’ ἐκπορευτῶς [The Holy Spirit is truly Spirit, going from (προϊὸν, a word that can correspond to the Latin procedens) the Father, not as a Son (οὐχ ὑϊκῶς) nor indeed as begotten (γεννητῶς) but as originating (ἐκπορευτῶς)].
 15. St. Gregory of Nazianzus, Oration 31 on the Holy Spirit, in Patrologia Graeca, ed. by J.P. Migne, vol. 36, D’Ambroise, Paris 1858, X, PG 36, 141 C: Τὸ πνεῦμα τὸ ἅγιον, ὃ παρὰ τοῦ πατρὸς ἐκπορεύεται· ὃ καθ’ ὅσον μὲν ἐκεῖθεν ἐκπορεύεται, οὐ κτίσμα· καθ’ ὅσον δὲ οὐ γεννητόν, οὐχ υἱός· καθ’ ὅσον δὲ ἀγεννήτου καὶ γεννητοῦ μέσον θεός: [The Holy Spirit, ‘who has his origin in the Father’ [John 15:26], who inasmuch as he has his origin in him, is not a creature. Inasmuch as he is not begotten, he is not the Son; inasmuch as he is the middle of the Unbegotten and the Begotten, he is God].
 16. Pontifical Council for Promoting Christian Unity: The Greek and the Latin Traditions regarding the Procession of the Holy Spirit and same document on another site
 17. Such as St. Gregory of Nazianzen, as seen in the passage from Oratio 39 cited above.

MarejeoEdit

 • Ayres, Lewis (2006). Nicaea and Its Legacy. Oxford: Oxford University Press. ISBN 0-19-875505-8. 
 • A. E. Burn, The Council of Nicaea (1925)
 • G. Forell, Understanding the Nicene Creed (1965)
 • Kelly, J. (1982). Early Christian Creeds. City: Longman Publishing Group. ISBN 0-582-49219-X. 

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.