Karadoki (pia: Karadawc, Caradog, Caratacus, Caractacus; alizaliwa Brycheiniog, Wales, karne ya 11 - Haroldston, 1124) alikuwa mwanamuziki aliyekuwa anapiga kinubi katika ikulu wa mfalme Rhys ap Tewdwr (1077-1093).

Kisha kuachana naye, kwa kuona mbwa wanatiwa maanani kuliko binadamu, alijiunga na Kleri ila baada ya miaka michache akawa mkaapweke, halafu padri na mmonaki [1][2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu, hasa tarehe 13 Aprili[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.