Kareyce Fotso ni mwimbaji wa Cameroon anayetumbuiza duniani kote na katika mitindo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Afro pop, blues na mangambeu. Ni mwimbaji wa kiafrika anayetunga nyimbo zake kulingana na tamaduni zilizomkuza.[1]

Kareyce Fotso
Amezaliwa
Bandjoun
Nchi Cameroon
Kazi yake Mwimbaji

Maisha hariri

Fotso alizaliwa Bandjoun akakua katika mji wa Yaoundé. [2] Huko Yaoundé alijifunza kuzungumza Ewondo na mara nyingi hutumbuiza katika lugha hiyo. [2]

Fotso alisoma biokemia na filamu shuleni, lakini hatimaye aliendelea kuwa mwimbaji. [3] Fotso aliimba kwenye bendi, Korongo Jam, kuanzia mwaka 2001, hadi bendi ilipogawanyika mwaka 2006.[2] Fotso alirudi Cameroon baada ya mpasuko ambapo alianza kutumbuiza katika cabarets huko Yaoundé.[2][4] Albamu yake ya kwanza, Mulato ilitolewa ndani ya nchi mwaka 2009.[2] Mwaka 2009 Jeux de la Francophonie, alishinda medali ya fedha katika mashindano ya wimbo.[5] Mwaka 2010 aliachilia albamu yake ya, Kwegne. [4] Albamu yake iliyofata, Mokte, iliachiliwa mnamo mwaka 2014. [6]

Fotso anaimba katika mitindo mbalimbali ikijumuisha mangambeu, Afro pop, miziki ya dunia, miziki ya taratibu na miziki ya kikabila. [6] Anapoimba, mara nyingi huambatana na gitaa, ngoma za mbao au kengele [3] Fotso anatumbuiza duniani kote. [6][7]

Marejeo hariri

  1. https://www.africaradio.com/news/kareyce-fotso-131952
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 Bessem, Frank. "Cameroon : Kareyce Fotso". Frank Bessem's Musiques d'Afrique (kwa Kiingereza). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 March 2017. Iliwekwa mnamo 2018-07-30.  More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); Check date values in: |archivedate= (help)
  3. 3.0 3.1 "Kareyce Fotso". Festival International Nuits d'Afrique de Montréal (kwa Kiingereza). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 September 2015. Iliwekwa mnamo 2018-07-30.  More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); Check date values in: |archivedate= (help)
  4. 4.0 4.1 "Découvrez Kareyce Fotso : l’une des voix les plus talentueuses d’Afrique", AfrikMag, 2017-02-03. (fr-FR) 
  5. "La parole à Kareyce Fotso…". Jeux de la francophonie (kwa Kifaransa). 27 March 2017. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 July 2018. Iliwekwa mnamo 2018-07-30.  Check date values in: |date=, |archivedate= (help)
  6. 6.0 6.1 6.2 "Kareyce Fotso: Ma musique est d'abord Camerounaise", Voila Moi, 2017-07-04. (fr-FR) 
  7. Webb, Genea L.. "Acoustic Africa: Afropean Woman Features Several Genres of Music", New Pittsburgh Courier, 21 November 2012. Retrieved on 2021-03-27. Archived from the original on 2018-11-18. 
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kareyce Fotso kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.