Katekista
Katekista ni Mkristo anayetoa katekesi, yaani ufafanuzi wa mpango wa imani, akitumia kwa kawaida kitabu rasmi maalumu kinachoitwa katekisimu, mbali ya Biblia ya Kikristo.
Majina hayo yanatokana na kitenzi cha Kigiriki κατηχεῖν (maana yake "kufundisha kwa sauti") ambacho ni mnyambuliko wa ἠχεῖν ("kufanya isikike").
Ujumbe wenyewe unaeleweka kuwa hasa Injili kadiri ya imani ya Kanisa, yaani yale ambayo lenyewe "linaungama, linaadhimisha, linaishi na linasali kila siku" (Papa Yohane Paulo II).
Kazi ya katekista inafuata ile ya kutangaza mbiu ya Injili kwa watu ili waone jinsi habari njema ya kifo na ufufuko wa Yesu ilivyo muhimu kwao, hasa upande wa wokovu.
Kwa kawaida kazi ya katekesi inaongoza waamini kwenye sakramenti mbalimbali, kuanzia ubatizo.
Mara nyingi katekista ni mlei anayejitolea katika parokia yake kisha kupata kozi maalumu hata ya miaka.
Chuo cha katekesi cha kwanza kilianzishwa na Panteno huko Aleksandria (Misri) mwishoni mwa karne ya 2, kikapata sifa hasa chini ya uongozi wa waandamizi wake, Klemens wa Aleksandria na Origenes.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Katekista kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |