Ban Ki-moon

Mwanasiasa na mwanadiplomasia wa Korea Kusini

Ban Ki-moon (* Eumseong, Korea, 13 Juni 1944) alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa tangu tarehe 1 Januari 2007 hadi 31 Desemba 2016 akimfuata Kofi Annan.[1]

picha ya Ban Ki-moon yamwezi wa pili,2016

Ban aliwahi kuwa Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini kati ya miaka 2004 na 2006. Tarehe 13 Oktoba 2006 alichaguliwa na Mkutano Mkuu wa UM kuwa Katibu Mkuu.

Mwaka 2013, jarida la Fobres la nchini Marekani lilimtaja Ban kuwa mtu wa 32 mwenye nguvu duniani na kuwa wa kwanza katika Korea Kusini. Mwaka 2014 alitajwa kuwa mtu wa tatu mwenye nguvu Korea Kusini baada ya Lee-Kun hee na Lee-jae yong.

Ban alisoma katika Korea Kusini hadi digrii ya kwanza ya B.A. kwenye chuo kikuu cha Seoul (1970). Mwaka 1985 aliongeza digrii ya uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Harvard (Marekani).

Familia

hariri

Ban alioa mke aitwaye Yoo Soon-taek na kuzaa mvulana mmoja na mabinti wawili. [2]

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Kigezo:Katibu Mkuu wa UN

  1. "Ban named next U.N. secretary-general". AP. Iliwekwa mnamo 2006-10-13. {{cite web}}: Italic or bold markup not allowed in: |publisher= (help)
  2. "Biography of the Minister of Foreign Affairs and Trade". Republic of Korea - Ministry of Foreign Affairs and Trade. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-08-06. Iliwekwa mnamo 2006-09-29. {{cite web}}: Italic or bold markup not allowed in: |publisher= (help)