Maeneo bunge ya Kenya

Maeneo bunge ya Kenya yanatumika kuchagua wajumbe wa bunge la Kenya. Kuna maeneo bunge 290 nchini Kenya.

Kenya ina mfumo wa kupiga kura wa mshindi-mmoja, kumaanisha kila eneo bunge linachagua mbunge mmoja tu.

Maeneo bunge yamegawanywa zaidi katika kata, zinazotumika kuchagua madiwani kwa serikali za mitaa.

Wabunge na madiwani wanachaguliwa wakati wa uchaguzi mkuu unaofanyika kila baada ya miaka mitano. Uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2007 ulisababisha mgogoro mkubwa.

Baada ya hapo ilitungwa katiba mpya ya mwaka 2010.

Maeneo bunge kaunti kwa kaunti

hariri

Viungo vya nje

hariri