Kepler (chomboanga)

Kepler ni darubini ya anga-nje iliyorushwa angani na taasisi ya NASA (Marekani) kwa shabaha ya kugundua sayari za nje zinazozunguka nyota nje ya mfumo wa Jua letu.[1]

Kepler ilivyochorwa na msanii.

Jina lilichaguliwa kwa heshima ya mwanaastronomia Mjerumani wa karne ya 17 Johannes Kepler,[2]

Kepler ilirushwa katika anga-nje tarehe 7 Machi 2009.[3]

Kazi yake ni kupeleleza sehemu ya Njia nyeupe na kugundua sayari za nje hasa zile ambazo zinazunguka nyota zake kwa umbali wenye uwezekano wa kuwa na uhai.[4] [5]

Data za Kepler zililenga kutambua nyota zinazoonyesha mabadiliko ya kurudiarudia ya angavu ya nyota zinazosababishwa na sayari zinazopita mbele ya nyota wakati wa kuangaliwa. Yaani kila sayari ikipita nyota yake inapunguza kiasi kiwango cha nuru kinachoonekana na mtazamaji wa nyota hii inaweza kupimwa.[6][7]

Kwa jumla Kepler ilikusanya data za nyota zaidi ya 500.000. Kutokana na utahmini ya data zake inaaminiwa leo kwamba asilimia 20 hadi za nyota zinazoonekana angani zinaweza kuwa na sayari ndogo zinazoweza kufanana na Dunia.

Kepler kumaliza kazi

hariri

Chomboanga hicho hakikuweza kuendelea na kazi yake jinsi ilivyopangwa kwa sababu kulitokea tatizo la kulenga tena darubini pale panapotakiwa [8]. Mwaka 2014 mbinu ulipatikana kuangalia tena magimba kwenye ekliptiki.[9]. Mwaka 2018 Kepler ilifika mwisho wa uwezo wake baada ya kuishia fueli yote.[10]

Marejeo

hariri
  1. Koch, David; Gould, Alan (2009). "Kepler Mission". NASA. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-03-06. Iliwekwa mnamo 2009-03-14.
  2. DeVore, Edna. "Closing in on Extrasolar Earths", SPACE.com, 2008. Retrieved on 2009-03-14. 
  3. NASA Staff. "Kepler Launch". NASA. Iliwekwa mnamo 2009-09-18.
  4. NASA Staff. "Kepler Mission/QuickGuide". NASA. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-08. Iliwekwa mnamo 2011-04-20. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |https://www.webcitation.org/67VwWtmA1?url= ignored (help)
  5. AAS Staff. "Meeting Program and block schedule". American Astronomical Society. Iliwekwa mnamo 2011-04-20. – click the itinerary builder to get to the abstract of "Kepler planet detection mission: Introduction and first results".
  6. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-06-03. Iliwekwa mnamo 2017-04-25.
  7. News (2012). "NASA approves Kepler mission extension". kepler.nasa.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-05-13. Iliwekwa mnamo 2017-04-25. {{cite web}}: |author= has generic name (help); Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |https://web.archive.org/web/20130513003153/http://kepler.nasa.gov/news/index.cfm?FuseAction= ignored (help)
  8. Kepler: Nasa retires prolific telescope from planet-hunting duties. BBC News Science & Environment, 2013. [1]
  9. Kepler Mission Manager Update: K2 Has Been Approved Archived 30 Novemba 2019 at the Wayback Machine., tovuti ya NASA ya 16-05-2014
  10. NASA Retires Kepler Space Telescope, tovuti ya NASA ya tar. 30-10-2018