Kichochezi (pia kichocheo, kwa Kiing. catalyst) ni istilahi ya kemia inayotaja dutu ambayo hu­badilisha kasi au kima cha mmenyuko wa kikemia (au utendanaji, Kiing. reaction) na yenyewe isiathiriwe wala kubadilika mwanzo hadi mwisho[1].

Mfano wake ni ukitia oksidi ya manganisi (MnO2) kwenye peroksidi ya hidrojeni (H2O2) ambayo itaanza haraka kuvunjika kuwa maji na oksijeni, ilhali MnO2 inabaki.

Kichochezi ndani ya michakato ya kikemia ya mwili huitwa kimeng'enya.

Kinyume chake ni kiviza, yaani dutu ambayo huzuia au hupunguza mwendo wa mmenyuko.

Marejeo hariri

  1. linganisha makala ya KAST
  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kichochezi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.