Kihungaria
Kihungaria (pia: KiMadyar, Kihungaria: magyar au magyar nyelv) ni lugha ya Kiugori ya magharibi katika jamii ya lugha za Kifini-Kiugori.
Huzungumzwa hasa katika nchi za Hungaria (10 mill.), Romania (1.4 mill.), Slovakia (520.000), Serbia (300.000), Austria (22.000), Australia (50.000) na Marekani (1.6 mill. - 117.000).
Kihungaria kama lugha rasmi au lugha inayotambuliwa
haririKihungaria kinatumiwa kama lugha rasmi kitaifa katika nchi zifuatazo:
Kinatambuliwa kama lugha ya wakazi wenye utamaduni wa Kihungaria katika nchi zifuatazo:
- Transsylvania (Romania) - katika Romania kuna lahaja ya pekee iliyoatiriwa na Kiromania huitwa "csángó" (tamka: chango).
- Slovakia
- Ukraine
- Kroatia
- Burgenland (Austria)
Ni pia lugha rasmi katika Umoja wa Ulaya.
Lugha inayofundishwa
haririKihungaria kama lugha ya kigeni kinafundishwa shuleni au kwenye taasisi za elimu ya watu wazima katika nchi nyingi. Mwaka 2001 idadi ya wanafunzi wa Kihungaria ilkuwa kama ifuatayo:
- Romania: 1.443.970
- Slovakia: 520.528
- Serbia: 293.299
- Ukraine: 149.400
- Marekani: 117.973*
- Kanada: 75.555
- Israel: 70.000
- Austria: 22.000
- Kroatia: 16.500
- Slovenia: 9.240
Jumla: watu milioni 12-13
Sauti
haririAlfabeti
a, á, b, c, cs, d, dz, dzs, e, é, f, g, gy, h, i, í, j, k, l, ly, m, n, ny, o, ó, ö, ő, p, q, r, s, sz, t, ty, u, ú, ü, ű, v, w, x, y, z, zs.
- ny = n+y (nyúl [nyuul] =sungara)
- gy = d+y (gyerek [dyerek] =mtoto)
- ly = y (hely [hey] = mahali)
- ty = t+y (tyúk [tyuuk] =inghoko)
- cs = ch (család [chalaad] =familia, jamaa)
- sz = s (szép [seep] =zuri)
- s = sh (sajt [shayt] =jibini)
- dzs = j (dzsem [jem] =kubana)
- zs = zh (zseb [zheb] =mbosho) - kama Kifaransa j wa jour
Uangalifu!
- di, ni, ti = [dy, ny, ty]
- gyi, nyi, tyi = [dyi, nyi, tyi]
- de, ne, te = [de, ne, te]
- gye, nye, tye = [dye, nye, tye]
Vitenzi
hariri
|
|