Kijiji cha Makumbusho Dar es Salaam

Kijiji cha Makumbusho Dar es Salaam ni eneo linalohifadhi mifano ya nyumba na vifaa vya tamaduni mbalimbali zinazopatikana katika nchi ya Tanzania.

Eneo hilo lipo katika jiji la Dar es Salaam, wilaya ya Kinondoni. Kijiji cha Makumbusho kipo mkabala na barabara ya Ally Hassan Mwinyi nje kidogo ya mji.

Kijiji hicho kilianzishwa mwaka 1966 kwa ajili ya kuonyesha na kutunza tamaduni, vikiwemo tamaduni za asili, ngoma na tamaduni za makabila mbalimbali kama Wanyakyusa, Wamakonde, Wamasai, Wachagga, Wahaya, Wangoni, Wayao na mengine mengi.