Wayao ni kabila la Kibantu kutoka eneo la karibu na Ziwa Nyasa.

Kinyago, Malawi

Mwaka 2001 idadi ya Wayao ilikadiriwa kuwa 1,942,000, ambao kati yao 1,000,000 wanaishi Malawi, 450,000 ni wakazi wa Msumbiji, na 492,000 wako Tanzania [1]

Wayao ni miongoni mwa Wabantu wanaopatikana katika mataifa kadhaa barani Afrika na kwa ujumla wao wameenea Malawi, Msumbiji na Tanzania katika mikoa ya Mtwara na Ruvuma.

Wakipatikana zaidi katika eneo kati ya Ruvuma na karibu na mto Lugenda kaskazini mwa Msumbiji.

Wanasifika sana kwa kuwa na utambulisho wenye nguvu wa kiutamaduni unaovuka mipaka.

Shughuli yao kubwa ni kilimo cha hapa na pale.

Upande wa lugha Wayao wenyewe wanaongea Kiyao; vilevile wanazungumza lugha rasmi ikiwamo ile ya Kiswahili kwa wale waliopo Tanzania, Kiingereza kwa wale wa Malawi na Tanzania na Kireno kwa wale waliopo nchini Msumbiji.

Wengi wao ni waumini wa dini ya Uislamu.

Miongoni mwao waliopata umaarufu mkubwa ni pamoja na marais wawili wa zamani wa Malawi: Bakili Muruzi pamoja na Joyce Banda.

Historia

hariri

Waarabu walipokuwa wakiwasili pwani ya Afrika walianza kufanya biashara na Wayao kwa kubadilishana nguo na bunduki na bidhaa za pembe za ndovu na watumwa; hivyo walikuja kuwa matajiri na kuwa kabila linalovutia barani Afrika.

Kukua kwa kabila la Wayao kulikuja baada ya kuchukua kwa mkoa wa Niassa huko Msumbiji katika karne ya 19. Tangu hapo Wayao walianza kuondoka katika makazi yao ya kiutamaduni, ambayo yalikuwa Malawi na Tanzania ya leo, hali iliyopelekea kusambaa kwa kabila hilo nchini.

Baada ya vita vya kwanza vya dunia katika karne ya 20 kabila la wayao lilijikita katika dini ya Uislamu kufuatia biashara iliyokuwepo kati ya Waswahili na Waarabu ambapo machifu walihitaji wenyeji wenye uwezo wa kusoma na kuandika.

Waalimu wa Kiislamu walioajiriwa kuishi katika vijiji vya Wayao walifanikiwa kueneza dini yao kupitia mafunzo mbalimbali waliyowapa Wayao ikiwemo elimu, vitabu vya dini, mavazi ya dini ya Kiislamu na nyumba zenye pembe badala ya zile za mduara.

Hata hivyo kiongozi wa Wayao alipambana kwa nguvu zote na ukoloni wa Wareno, Waingereza na Wajerumani lakini pia utawala wowote wa kikoloni ambao ulionekana ni tishio kwa uchumi wake.

Chifu wa Wayao Mataka aliupinga Ukristo kwani Waislamu waliwapa mahitaji yao ya kijamii ambayo yaliwafaa kwa tamaduni zao, kwa sababu siasa na ibada ya utawala wa machifu, uongofu wao kwa Uislamu ulisababishwa masomo yao kufanya Vivyo hivyo.

Wayao wa Msumbiji

hariri

Walikuwa wakiishi kaskazini mwa taifa hilo lililotawaliwa na Wareno. Ukiangalia kwa ukaribu historia ya Wayao wa Msumbiji katika jiografia yao ipo katika kijiji kidogo cha Chiconono, katika jimbo la Niassa, kaskazini magharibi mwa Msumbiji.

Nao ni wakulima wa hapa na pale ingawaje vilevile walikuwa wamejikita kwenye uuzaji biashara ya pembe za ndovu na biashara ya watumwa.

Walikumbwa na anguko la kisiasa na kiuchumi baada ya Wareno kufika katika jimbo la Niassa ambako walianzisha kampuni ambapo walijenga makazi na kuvunja mashamba na kuharibu biashara na kubadilisha kuwa uchumi unaotegemea mazao uliokuwa ukichungwa na Wareno.

Kupanuka kwa himaya ya Kireno kulianzisha kituo muhimu cha biashara, ngome ya jeshi, na bandari tangu karne ya 15 kiasi cha kuwavutia majeshi ya Waislamu, wakiwamo Wasomali na Waswahili.

Misafara ya Wareno na uenezwaji wa dini ya Ukristo ndio kuliwafanya zaidi Wareno kujitanua ingawaje baadaye (karne ya 19) Wareno walikuja kujihusisha na biashara ya utumwa kutoka Msumbiji hadi Brazil.

Himaya ya Wareno kwa wakati huo ilikuwa tawala kubwa kisiasa na kiuchumu duniani, kwa wakati huo walikuwa wakiendesha kilimo kilichopata mafanikio kwa kuwalipa makundi makubwa ya wakulima ya makabila, na katika kundi la Wayao uzalishaji wao ulikuwa chini ya uongozi wa Wareno.

Ingawaje Wayao walikuwa wanaenzi mila na tamaduni zao, namna ya kilimo chao cha hapa na pale, kama waisali Wayao hawakuzisimamia na kujikuta wameanza kufunzwa elimu ya Ukristo, na kuanza kufundisha lugha ya Kireno kwa Waislamu.

Kwa sasa, Wayao wanaoishi Msumbiji wanakadiriwa kufikia 450,000, ambao ni asilimia 40 za wakazi wa Lichinga.

Wayao nje ya Msumbiji

hariri

Miaka ya 1830 Wayao, wakiwa wafanyabiashara na wakulima, walianza kuenea mashariki mwa Malawi, ambako walikuwa matajiri katika mila na muziki ambao wengi wao walikuwa Waislamu.

Wayao walikuwa na mahusiano ya karibu na Uswahili katika pwani wakati wa karne ya 19, na kukubaliwa baadhi ya maeneo ya utamaduni wao, kama vile usanifu na Uislamu.

Wayao walikuwa na uhusiano wa karibu na Waswahili wa pwani katika karne ya 19 na kuiga baadhi ya tamaduni zao, ikiwamo usanifu na Uislamu, ingawaje waliendelea utamaduni wao wa kitaifa.

Ushirikiano wao na Waarabu uliwapa fursa ya kupata silaha za moto ambazo walizitumia katika vita baina yao na Wangoni na Wachewa. Wayao walikuwa wapinzani wa utawala wa Wajerumani kusini mwa Afrika katika eneo la Tanzania, Rwanda na Burundi za leo.

Wayao wa Tanzania

hariri

Wayao, ambao jina la kabila lao linatokana na "mlima Yao" katika nchi ya "Unangwa" huko Msumbiji, kati ya mto Lujendo na ziwa Nyasa. Waligawanyika katika koo nyingi ambazo ni Amasaninga, Amangochi, Amalambo, Wamakale, Wambemba, Wankula, Wanjese, na Achingoli.

Hapo awali Wayao walijulikana kwa jina la "Akinankunde", waliishi "Kumbemba" Msumbiji. Hapo aliishi mtu mmoja aliyeitwa Kawina ambaye alimposa binti wa ukoo wa "Akinankunde". walimzaa mtoto ambaye alisababisha vita akampindua baba yake aliyelazimika kuhamia "Unangu" na kuishi huko mpaka alipovamiwa na Wangoni hapakuwepo mshindi.

Baada ya muda, Wayao walioishi Unangu walitelemka kutoka milimani na kuishi kwenye sehemu zilizokuwa tambarare. Mnamo karne ya 15 Wareno walipoivamia nchi ya Wayao na kuwataka kuamini dini yao ya kigeni, wazalendo walizigundua njama zao za kutaka kuwatawala, hivyo wakapanga kuwapiga vita. "Chemataka" akiwa ndiye kiongozi wao shupavu alitumua kla njia ili apate ushindi kwa bahati mbaya aliishiwa baruti.

Ndipo ikamlazimu atume ujumbe wa watu 36 ulioongozwa na "Kadewele" kwa Waarabu waliokuwa wanaishi ng'ambo ya pili ya mto Ruvuma. Kwa kuwa Kadewele alikuwa mtumwa, hakuwa na la kufanya ila kutii.

Kadewele akifuatana na "Mandingo", Mbunda, Makelele, Kachoko na akina Mkubango aliuvuka mto Ruvuma na kufika Sasawala kwa Mkupeni. Hapo hapakumpendeza, hivyo akahamia na kufanya makazi yake kando ya mto Tunguru.

Hata hvyo Waarabu hawakuamini kama Che Mataka alikuwa na nia ya dhati ya kuomba msaada kwani alikuwa amemtuma mtumwa tu. Che Mataka alipopata habari hizo aliamua kumtuma mama yake mzazi "Bibi Kundenda" binti Kawina avuke mto na kuomba msaada.

Kadewele alipoona mama yake sultani Che Mataka amefika akahisi kuwa kusudi la Bibi Kundenda lilikuwa ni kumrudisha utumwani, hivyo ilimpasa kutoroka na kuhamia mahali palipoitwa "Tunduru" tarehe 14 Aprili 1901.

Jina Tunduru linatokana na ukoo wa Machemba ambaye alikuwa mtawala na mke wake aliyekuwa bibi mkubwa aliitwa "Akwitunduru". Mpelelezi wa Kidachi wa kwanza Linder alimkuta Kadewele akiishi Akwitunduru na akashindwa kutamka neno Akwitunduru akatamka "Tunduru" ndipo jina la eneo ilo lilivyopatikana.

Kadewele alipokuwa akimkimbia Bibi kundenda alifika mahali palipoitwa "Mlingoti" ambapo sasa panajulikana kwa jina la Nanjoka, aliamua kuishi hapo. Jina Mlingoti lilitokana na Wangoni, kwa sababu walipofika hapo walivutiwa na miti mirefu iliyokuwepo, walipumzika na kupiga kambi. Miti hyo waliita Mlingoti.

Kadewele na kikundi chake waliishi Mlingoti wakiwa wawindaji maarufu na uku Mandingo akiwa anaishi eneo jirani karibu na mto Nanjoka mpaka sasa panajulikana Kama Mandingo. Ili Kadewele ajikomboe kutoka utumwani alimpelekea Bonomali Mataka zawadi ya meno ya tembo aliyekuwa mkubwa sana. Inasemekana fuvu la tembo huyu lilipelekwa Dar es Salaam na Mjerumani mmoja aliyetokea Lindi. Baadhi ya mifupa ya tembo huyo imewekwa kwenye jumba la makumbusho Dar es Salaam

Vita vya Majimaji vikatokea Songea vikamkuta mwinyi Kadewele akiishi Mlingoti. Sultani Mataka aliposkia juu ya vita hivi alituma askari 70 ili wafike kumlinda mama yake Bibi Kundenda. Wapiganaji wa vita vya Majimaji walipomshauri Kadewele kunywa maji, Kadewele hakusita kwani alitambua wazi kuwa

  • "umeshatolewa wito, kwa Wayao"
  • kwamba wawe motomoto, ili waweze komboka
  • wawe na chao kimeto, cha toka hiyo miaka
  • kama kufa ilibidi, hakuwa na la kuacha."

Taarifa hii haikukawia kuwafikia Wajerumani huko Lindi na muda si mrefu Mwinyi Kadewele na wenzake kina Kitambi na Mwenda walitiwa mbaroni.

Kifo cha kishujaa kiliwafikia wakiwa gerezani Lindi. Ukurasa mpya ukawa umefunguliwa.

Baada ya Wajerumani wakaamua kujenga ngome yao ya kuwatishia wananchi huko Tunduru. Huo ulikuwa mwanzo wa ukoloni mkongwe.

Mnamo mwaka 1910 Wajerumani walimruhusu kwa hila Chisonga Msenda" ajenge ikulu yake huko Nampungu. Mfumo huo wa utawala wa jadi ulifanana sana na ule wa nchi yao ya asili kwa kuwa kila aliyetawazwa alitunukiwa cheo cha Che Mataka. Hata hivyo kile kilikuwa ni kilemba cha ukoka kwani mkoloni alikwishajitwalia madaraka na kumnyang'anya Myao haki za kujitawala. Dhuluma hiyo haikumwelemea Myao tu bali makabila yote ya Tanganyika.

Tanbihi

hariri
  1. [1].
  Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wayao (Tanzania) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.